ujasiriamali June 2015 - UJASIRIAMALI
Education

SULUHISHO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

02:47

Ukweli ni kwamba ndoa nyingi za Kikristo zinavunjika kutokana na tatizo hili. Je, hakuna haja ya kuitisha mjadala wa kitaifa? Taifa letu linaangamia kwa kukosa maarifa.

Hivi upungufu wa nguvu za kiume ni nini? Kifupi ni mwanamume kutokuwa na uwezo wa kutoa mbegu bora zenye uwezo wa kutungisha mimba, au kutosimama kwa uume.

Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya wanandoa nchini wanakabiliwa tatizo hili. Kwa hiyo, mabango ya waganga yaliyopo barabarani hayajapunguza kabisa tatizo hilo.

Hawa watu wanatibu watu au majini? Hapo ndipo kiini cha makala haya. Sababu kubwa ya ongezeko la wenye matatizo haya ni kwamba dawa nyingi zinazodaiwa kuponya tatizo hili hazina viwango vya kuitwa dawa, bali ni vichocheo tu kwani kinachopigiwa chapuo huwa ni kumudu tendo kitandani na si nguvu asilia.

Waganga wengi wameelekeza nguvu zao huko na ni hapo ndipo janga hili la kitaifa linapoota mizizi.

Ukweli ni kwamba upungufu wa nguvu za kiume hauondolewi kwa dawa za kuchochea nguvu wakati wa tendo. Hizi zina madhara makubwa na mara kadhaa husababisha vifo kwa wanamume wengi wakiwa ‘guest’ na vimada wao kwani hulipua moyo.

Ni lazima kiini cha tatizo hili kichunguzwe na tiba stahiki ipatikane. Kinyume cha hapo, janga hili linaweza kugeuka na kuwa dubwana kubwa la kutumaliza.

Matatizo ya nguvu za kiume huchangiwa na kuugua kwa muda mrefu, ugonjwa wa kisukari, kuvaa nguo za kubana sana, mionzi ya simu, kompyuta na mengineyo. Pia dawa za kuua wadudu huleta tatizo hili kwani zina viambata sumu viitwavyo ‘estrogen’, matatizo ya kisaikolojia, kupiga punyeto kwa muda mrefu na kutumia vyakula vyenye kemikali.

Utafiti unasema kuna uhusiano mkubwa sana kati ya upungufu wa nguvu za kiume na kuwa na sumu mwilini zinazotokana na vyakula vyenye kemikali tunavyobugia kwa kupenda au kutokupenda.

Ni kutokana na utafiti huo ndipo dawa bora yenye uwezo mkubwa wa kuondoa sumu mwilini kwa muda mfupi ikagunduliwa. Hii ikiwekwa kwenye kinywaji chochote chenye kemikali, mara moja hutenganisha sumu iliyomo humo.


Dawa hii pia huleta nguvu za kudumu za kiume, hujenga afya na kuleta nguvu asilia. Hutatua tatizo la nguvu za kiume huku ukiondoa pia tatizo la ugumba na ni vizuri wenye matatizo kama hayo wakatumia vyakula vya protini hasa ya mimea kwani hurutubisha mbegu.

Kuna aina 2 ya vyakula ambavyo vimefanyiwa utafiti na kubaini kuwa ni moja ya vyakula vinavyosaidia kuongeza nguvu za kiume na havina madhara katika engezeko la nguvu za kiume, katika vyakula hivyo vyenye uwezo wa kuongeza nguvu za kiume kiasili ni:

1. TANGAWIZI

- Tangawizi ni moja ya chakula kinachoweza kurejesha nguvu za kiume, unaweza kuichemsha tangawizi na ukatumia kwa kuinywa kama chai Asubuhi, mchana na jioni pia Tangawizi unaweza ukaitumia katika mchanganyiko wa kiasili kwa kutumia habat soda,asali,kitunguu saumu na tangawizi yenyewe.

JINSI YA KUTUMIA MCHANGANYIKO HUU: Chukua tangawizi na kitunguu saumu vitwange kisha vichanganye na asali pamoja na unga wa habat soda na uwe unakunywa mchanganyiko huu kwa kutumia kijiko cha chai kimoja kutwa mara 3 kwa muda wa wiki moja na utaona mabadiliko.

2. TIKITI MAJI:
Chakula kingine kinachosaidia katika upande wa kuongeza nguvu za kiume ni tunda la Tikiti Maji, unaweza ukachukua tikiti lako ukalikata na kutengeneza juice ya Tikiti kisha unakunywa ila sio lazima utengeneze Juice hata lenyewe tu unaweza ukalila. Ila jitahidi kutumia tunda hili hata kila siku kwani linasaidia sana kwa wenye matatizo ya nguvu za kiume.

Education

MAMBO 6 YAKUZINGATIA KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI

02:14

Mara nyingi wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile ya awali wakati mnaanza mapenzi yenu.  Wanawake wengi wanalalamika kuwa  hawaoni upendo ule waliouzoea zamani wakati mapenzi yanaanza. Hata wanaume wengine wanalalamika pia kuwa penzi limeteremka kiwango baina yao.
Mara zote hushuka huku kwa ukaribu (intimacy) hakupangiliwi au kutazamiwa bali huja taratibu pasipo wapenzi kutambua, mara lugha hubadilika,  muda wakuwa pamoja hupungua, mambo huanza kufanywa kwa mazoea, vilivyo zoeleka kufanyika havionekani tena na taratibu hali hii ikikomaa huathiri hata tendo la ndoa. Katika hatua hii, wapenzi huanza kuchokana na kutotamaniana, hapa ndio kwenye upenyo wa mmoja au wote kuwaza njia mbadala.  Wengi walioachana au kutalikiana nao  walipitia njia hii pia.
Ili kuepuka yote haya, haunabudi kujifunza njia za kuwasha moto wa upendo kila wakati na kuongeza ukaribu (intimacy) kati yenu.
Njia za kukusaidia

1.       kucheka pamoja
Kicheko ni mlango wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia pamoja, na hapa mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu, kama waweza kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya katika vyote.  Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu.  Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea.  Kama utaanza kujizoeza  hivi ukiwa nyumbani, taratibu  utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine kokote.


2.       Jifunzeni kutiana moyo
Kila mmoja awe msaada na tegemeo kwa mwenzake.  Jifunze kumtia moyo na kumwezesha mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au apendavyo.  Onyesha heshima katika vitu hivyo pia.  Kila upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu.  Mjenge mwenzako mbele yawengine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye.  Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo.  Zaidi tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini na kutunyanyua  na sisi pia.

3.       Jifunzeni kupenda kugusana
Nguvu ya mguso wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote.  Lazima mjifunze kujenga tabia ya kugusana mara mpatapo nafasi sio tu mnapokuwa mmelala.  Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono mkiongea au mkitembea, kukumbatia bega, kugusa au kuchezea nyewele za mwenzako na njia nyingine zozote za kuonyesha ukaribu kimwili.   Wengi wetu huweza kufanya haya kidogo tunapokuwa peke yetu na kamwe sio mbele ya watu, Je, ni aibu? au nidhamu mbaya? au  dhambi?
Kugusana ndio mwanzo wakuamsha hisia za kuhitajiana, (hembu jiulize kisirisiri, lini umegusana na mwenzako nje ya chumbani). Kumgusa umpendaye hukuzuia kutowaza au kutovutiwa kumgusa yeyote katika ulimwengu uliojaa wengi waliopweke wanaotamani kuguswa.
Mguso huu wa upendo haumaanishi mguso wa tendo la ndoa, ingawa pia ni vema kujifunza kuijenga lugha ya mguso wa  tendo la ndoa katika  mahusiano yenu.


4.       Zungumzeni hisia zenu
Kati ya vikwazo vikubwa katika ustawi wa mahusiano mengi hususani ya wanandoa ni kutokuwepo kwa majadiliano.  Lazima wapenzi wajifunze kuzungumza kuhusu hisia zao.  Kama vile maisha yasivyo na ukamilifu, mahusiano na hata ndoa pia hazina ukamilifu.  Mpenzi wako hayuko kamili na wala wewe pia sio mkamilifu.  Jifunze kuzungumza na umpendaye jinsi unavyojisikia na nini kinachokusumbua. Kuendela tu na migogoro isiyosuluhishwa husababisha moyo kuwa baridi juu ya mwenzako, jiwekeeni muda kila wiki ninyi wawili kutoka ili kuzungumza mambo yenu.  Mwambie umpendae yapi yanayojiri kila siku na zipi changamoto zako, mkiweza kujifunza kuwekeza katika muda wa kuwa pamoja taratibu hata muda wenu wa maongezi ya simu utaongezeka.

5.       Samehe na kubali kusamehewa
Kamwe tusiache maumivu na machungu yatawale mahusiano yetu.  Lazima tujifunze kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia.  Kutofautiana katika mahusiano kupo sana, na lazima tuwape tuwapendao nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yetu.  Kila hisia za mmoja wetu zinaumuhimu.  Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako akuambie yanayo muumiza na msameheane.


6.       Linda muonekano wa mpenzi wako
Mara nyingi hatari hii hutokea tunapokuwa katika mizunguko ya huku na huko.  Ukaribu na mpenzi wako hauendelezwi tu bali pia unalindwa, pia muonekano  wetu lazima ume halisi na sio feki.  Vile tunavyoviona katika tamthilia na filamu sio ukaribu ulio halisi.  Kama tunataka tuonekane sawa na vile tunavyowaona wengine wanavyopendana basi tunakosea na kujizuia kuwa na mtazamo bora katika mahusiano yetu.  Ukianza kupata  ukaribu wa kweli baina yako na mwenzako utapoteza hisia ya kuhitaji ukaribu huo na mwingine yeyote, na badala yake utaanza kuulinda ukaribu mlionao.
Lengo liwe kuvitafuta vile vyote  mpenzi wako alivyonavyo ambavyo  hukuza ukaribu wenu.  Mwenzako awe ndio mtu wa muhimu kuliko wote katika maisha yako

Home

FACEBOOK YAFUNGUA OFFICE AFRICA KUSINI

23:08

Matarajio ya Kampuni ya Facebook ni kujizolea watumiaji wengi zaidi Afrika
Kwa mara ya kwanza Facebook imefungua ofisi yake barani Afrika, Johannesburg nchini Afrika kusini ikiwa ndio makao makuu.
Mwanadada Nunu Ntshingila ndie atakae ongoza ofisi hiyo itakayo jikita katika kutafuta njia mbali mbali za kuongeza ushirikiano na wafanya biashara wa barani humo.
Tayari watumiaji wa facebook barani Afrika ni milioni 120, ofisi hiyo mpya inalenga kuongeza idadi ya watumiaji wake nchini Kenya, Nigeria na Afrika Kusini.
Nunu Ntshingila ndiye mkurugenzi mkuu wa ofisi hiyo ambae amesema kuwa mkakati wa kupanua uwekezaji wao hasa katika matangazo ni mipango mikubwa ya kutanua biashara pamoja na bara la Ulaya na maeneo ya Mashariki ya Kati.
Barani Afrika kuna mtumiaji mmoja kati ya watano wa intanenti na inatarajiwa idadi hiyo kukua mara mbili zaidi kwa watumiaji wa simu za mkononi ifikapo mwaka 2020.
Asilimia 80% ya wanao tumia facebook ni wale wenye kupata huduma hiyo kupitia simu zao za mikoni.
Facebook anasema pia ina mipango madhubuti ya kuongeza wateja kutoka nchi za Senegal, Ivory Coast, Ghana, Tanzania, Rwanda, Uganda, Zambia, Msumbiji na Ethiopia ili kufikia malengo yake

KANTANKA MAGARI YANAYOTENGENGENEZWA GHANA

13:25


Wakati unapoangazia swala la utengezaji magari mataifa ya Afrika kwa kawaida hayaorodheshwi katika swala hilo.
Lakini hilo sasa huenda likabadilika kufuatia kuwasili kwa kampuni ya magari ya Ghana Kantanka ambayo hivi karibuni yataanza kuingia katika soko.
Miongoni mwa magari ya kampuni hiyo ni lile la lita mbili aina ya 4 by 4 ambalo linatarajiwa kuuzwa kwa takriban pauni 14,000.

Lakini je,kampuni hiyo itaweza kukabiliana na ushindani mkubwa kutoka kwa magari kama vile Toyota,Land Rover na BMW?.
Kwadwo sarfo ni mwana wa mmiliki wa magari hayo.
Babaake ni m'bunifu ambaye pia ni kiongozi wa dini.Hupata fedha kutokana na kilimo na uchimbaji.
Magari ya Kantanka yanafananishwa na magari makubwa kama vile Toyota Prado ama MItsubishi Pajero.

Mbele ya gari hilo kuna michoro ya kucha za chui pamoja na nembo ya kampuni hiyo ya nyota ya Afrika.
Kulingana na raia mmoja wa Ghana uvumbuzi kama huo haujafanyika nchini humo.
Tunapenda kununua bidhaa kutoka nje kwa hivyo italazimu kufanyika kwa mauzo ya ziada kwa gari hizi za kantanka kukubalika.
Profesa Robert Ebo Hinson ambaye ni mkuu wa kitengo cha mauzo katika chuo kikuu cha Ghana:Nadhani kile kilichotokea hapo awali ni kwamba tumefanywa tuamini kwamba kile kinachotengezwa katika mataifa ya magharibi ni

bora zaidi kwa sababu zote zile.
Wakati mwengine bidhaa zinazotengezwa kutoka Ghana haziwezi kudumu.
Serikali ya Ghana inaelewa kikwazo hicho na tayari imeanzisha kampeni kubwa ya kuwafanya wakaazi kununua bidhaa zinazotengezwa nchini humo.
Waziri wa biashara daktari Ekow Spio Gabrah anaongoza kampeni hiyo na anasema:Nitaendesha moja ya magari haya,kwa kweli niliketia gari moja wakati lilipokuwa likitengezwa na nafurahi kuwa na moja kama gari langu rasmi.

Waziri na rais wana uwezo wa kuendesha magari hayo kwa gharama ya walipa ushuru.
Lakini je,raia wataweza kutumia fedha zao wenyewe kulipia gharama za kulinunua gari hilo?
Inaonekana kwamba raia wengi kama alivyodai hapo awali Professa wana wasiwasi kuhusu usalama wa gari hilo na kudumu kwake.

Je, unadhani wasiwasi huo huenda ukaathiri uzalishaji wa magari hayo? Kulingana na Kwadwo Sarfo gari hilo la kwanza kutengezwa nchini Ghana litapata umaarufu.

PAKA ALIYEKUWA MKUU WA KITUO JAPANI AFARIKI DUNIA

05:26

Paka mmoja wa Japani ambaye alipata umaarufu alipofanywa kuwa mkuu wa kituo cha reli, amefariki, na waombolezaji wengi wamejitokeza.
Wakuu na washabiki walihudhuria mazishi ya paka huyo, katika kituo cha reli, ambako alitumika.
Paka huyo aliyejulikana kwa jina ''Tama'' ambaye alipatikana akiranda randa katika kituo cha reli cha Kishi miaka minane iliyopita kabla yake kutawazwa kuwa meneja wa kituo hicho,
aliaga dunia majuzi kutokana na umri wake mkubwa wa miaka 16.
Tama aliishi katika kituo hicho akiwa amevalia sare rasmi ya afisa mkuu wa kituo cha reli na kuibuka kuwa kivutio kikubwa cha watalii.
Alivishwa kofia na kikoti maalumu alichoshonewa.
Viongozi na wananchi wa matabaka mbalimbali walimmiminia sifa paka huyo hasa wakisema kuwa ndiye aliyefufua kituo hicho cha reli.
Rais wa shirika la reli ya umeme la Wakayama Japan , bwana Mitsunobu Kojima, alimsifu Tama kwa kufufua uchumi katika eneo zima la Wakayama.
'' Bi Tama, japo umetuacha ninakupa heshima na kuanzia leo utasalia kuwa mkuu wa kituo hich cha reli milele''alisema Kojima

Paka aliyehudumu kama mkuu wa kituo cha reli
tangazo hilo lilishangiliwa na waombolezaji waliofika katika maziko hayo.
Pengo lililoachwa na kifo cha bi Tama tayari limejazwa na paka mwengine mpya ambaye kwa sasa hajapewa heshima za kuwa mkuu wa kituo hicho.
Gavana wa kanda hiyo ya Wakayama , Yoshinobu Nisaka, amewashauri wadogo wake wamtunze mrithi wa Tama na vilevile wamfunze kazi.
''itakuwa bora sote tukichukua jukumu la kuendeleza utamaduni wa kihistoria ulioachwa na bi Tama''alisema gavana Nisaka.
Tama kama paka huyo alivyofahamika alilelewa na wafanyikazi wa reli katika kituo hicho cha Kishi.
Hata hivyo maisha yake yalibadilika shirika la reli lilipowafuta kazi wafanyikazi wote katika kituo hicho n hivyo akasalia humo asijue pa kwenda.
Tama baadaye alitambuliwa na wakuu wa shirika hilo na hivyo akatawazwa kuwa mkuu wa kituo hicho.
Umaarufu wake uliibua mtindo mpya wa mavazi ya paka,biashara ambayo hadi sasa inanogo katika eneo hilo la Kishi na Japan kwa jumla.
Aidha watalii walibadili safari zao na kupitia katika kituo hicho cha reli ilikujionea wenyewe ''afisa huyo mkuu'' akihudumia abiria.
Maajabu ya ulimwengu! http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/06/150628_cat_stationmaster_dies_japan?ocid=socialflow_facebook

Education

UNATAKA KUFANIKIWA KATIKA MAISHA ACHA TABIA HIZI:

16:30

Watu wengi mara nyingi huwa wanafikiri kukosa mafanikio ni matokeo ya kukosa bahati au ni matokeo ya mapungufu Fulani waliyonayo katika maisha yao, kitu ambacho siyo cha kweli. Kutokana na kuwa na fikra hizi, huwazuia  wengi kufanikiwa na kujikuta ni watu wa kulaumu na kushindwa kujua nini kinachowazuia wasiweze kufanikiwa wakati kila kitu cha kuwafanikisha wanacho.

Wengi hujikuta wakitafuta vitu vingi vilivyo nje yao na kusahau kitu kimoja kikubwa kinachowazuia mafanikio yao. Kitu hiki pekee kinachozuia sana mafanikio ya wengi ni tabia tulizonazo. Wengi wamekwama na kushindwa kuendelea sio kwa sababu hawana mtaji wala akili ni kwa sababu ya tabia zao. Tabia ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya mtu binafsi kuliko unavyofikiri.

Kama Unataka Kufanikiwa Na Kuwa Tajiri, Acha tabia Hizi:-

1. Acha tabia ya kuahirisha mambo.
Kama kuna jambo au kitu unachotakiwa kukifanya leoleo ni vizuri ukafanya kuliko kukiacha na kutegemea utafanya kesho. Wakati wa kubadili maisha yako upo sasa na wala si kesho kama unavyofikiri. Hiyo kesho unayoisubiri haitafika na wala hakuna kesho kama unavyofikiri. Ni mara ngapi umesema utafanya kitu hiki kesho na hukufanya? Hii ni moja ya tabia inayokuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa unayoyataka. Unataka kuwa tajiri achana na tabia hii kwanza.

2. Acha tabia ya kufikiria sana makosa uliyoyafanya.

Wengi wanakuwa wanashindwa kusonga mbele kutokana na kufikiria sana makosa waliyoyafanya siku za nyuma. Kama kuna sehemu ulikosea, hiyo imeshapita chukua hatua sasa za kusonga mbele. Acha kuumia na kung’ang’ania kufikiri pale ulipokosea, hiyo haitakusaidia sana zaidi ya kukurudisha nyuma. Kama ambavyo nimekuwa nikisema mara kwa mara kukosea ni sehemu ya maisha ya binadamu, kitu cha msingi jifunze kutokana na hayo makosa.

3. Acha tabia ya kuongelea sana ndoto zako.

Watu wengi sana ni waongeaji juu ya ndoto zao lakini sio watendaji. Kama ni kuongea umeongea sana juu ya ndoto zako, umefika sasa wakati wa kufanya mambo yako  kwa vitendo. Jifunze kuchukua hatua dhidi ya ndoto zako kila siku, hata kama ni kwa kidogo kidogo utasogea, mwisho utajikuta unafanikisha kile unachokitaka. Hii ni tabia ambayo imekuwa ikiwakwamisha wengi kutokana na kuongea sana. Unataka mabadiliko achana na tabia hii.

4. Acha tabia ya kutokujiwekea akiba.

Hii ni tabia ambayo ukiiendeleza katika maisha yako kutojiwekea kipato itakuwa ni ngumu sana kwako kufanikiwa. Unaposhindwa kujiwekea kipato katika pesa unayoipata kitakachokutokea katika maisha yako, utashindwa kumudu kupata pesa ya kuendeshea miradi yako na mwisho wa siku utakuwa ni mtu wa kulalamika tu. Kama unataka kuwa tajiri na kuwa huru kifedha anza kujifunza kujiwekea akiba, hii itakusaidia sana kusonga mbele katika mambo yako mengi.

5. Acha kutumia pesa zako hovyo.

Watu wengi huwa ni watumiaji vibaya wa pesa zao hasa pale wanapozipata. Unapotumia pesa zako hovyo hiyo hupelekea kuweza kukosa pesa ambayo ungeweza kuipata kama akiba yako ya baadae. Mtumizi mabaya ya pesa, ni moja ya tabia kama tabia zingine, lakini ambayo inakukwamisha kwa kiasi kikubwa kufikia ndoto na malengo yako makubwa uliyojiwekea. Ili uweze kusonga mbele na kuachana na majuto uliyonayo jifunze kutunza pesa zako vizuri, utafanikiwa.

 6. Tabia ya kuwa na madeni mengi.

Unapokuwa na madeni mengi hiyo itakusababishia badala ya kuendelea mbele utakuwa unarudi nyuma. Acha kulimbikiza madeni ambayo kwako yanakuwa mzigo kwako. Kabla hujakopa chukua hatua muhimu ya kujiuliza je, kuna ulazima wa kukopa hiyo pesa? Madeni ni kitu ambacho kimekuwa kinawarudisha wengi nyuma bila kujua, kutokana na kuwa na elimu ndogo inayohusiana na madeni. Unataka kuwa na mafanikio, iache tabia hii mara moja.

7. Tabia ya kusubiri sana kutekeleza ndoto zako.

Hakuna muda sahihi ambao upo wa kuanza kutekeleza ndoto zako kama unavyofikiri. Muda wa mafanikio na kufanya ndoto zako kuwa za kweli ni sasa na wala si kesho. Acha kuwa na tabia au fikra za kufikiri kuwa mipango yako mingi utaiyafanya siku nyingine, hakuna kitu kama hicho. Hii ni tabia ambayo umekuwa nayo na inakukwamisha. Unataka kutoka hapo ulipo anza kutekeleza mipango na malengo yako iliyojiwekea mara moja.

Kama una nia ya kweli kutaka kuleta mabadiliko makubwa katika maisha yako, anza kujiandaa kubadilika wewe kwanza ikiwa ni pamoja na kubadili hizo tabia ulizonazo zinakukwamisha sana. Kwa kadiri, utakavyoweza kumudu kubadili tabia zako kwa kiasi kikubwa, ndivyo utakavyo jikuta maisha yako yanakuwa na mafanikio makubwa kuliko unavyofikiri. Kumbuka hili, mafanikio yanajengwa na tabia tulizonazo.

Education

ATHARI ZA KULA MAYAI YASIYO IVA VIZURI

14:06

Mayai ni moja ya vyakula vyenye viini lishe muhimu kwa ajili ya afya ya mwili wa binadamu. Kwa kawaida mayai kabla ya kuliwa, huandaliwa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchemshwa, kukaangwa au kuchanganywa na vyakula vingine kama vipande vya viazi mviringo ambavyo ni maarufu kwa jina la chips.

Pia, kuna baadhi ya watu wanaopendelea kula mayai mabichi kama dawa ya tiba mbadala, kwa ajili ya kulainisha sauti na wengine hupendelea kula mayai ya kukaanga ambayo hayakukaushwa vizuri.

Ukitembelea migahawa mingi utabaini kuwa watu wanakuwa na mitazamo tofauti na wanavyopenda kula mayai.

Mfano kuna wanaoagiza watengenezewe mayai kwa mtindo unaojulikana kama ‘macho ya ng’ombe.’ Ukiagiza namna hiyo, mpishi atataka kuuliza kama ni ‘macho ya ng’ombe’ ya kugeuza.

Ina maana kuwa ‘macho ya ngombe’ ya kugeuzwa ni yale yanayoivishwa pande zote lakini yale ambayo siyo ya kugeuza, huwa linaifa nusu. Upande mmoja unabaki ukiwa mbichi, na ndiyo raha ya baadhi ya watu.

Hata ukienda kwa wakaanga chipsi, utakuta wanawauliza wateja wao kama wanapokaanga na mayai wakaushe au wasikaushe. Hii inaashiria kuna watu wanataka wale chipsi zikiwa na mayai ambayo halijaiva sawasawa.

Kuna watu wengine wanaamini kwamba kula mayai mabichi kunafanya sauti inakuwa nyororo, hivyo wale waimbaji huwalazimu kufanya hivyo ili kufanya nyimbo zao zivutie.

Si hivyo tu, kuna baadhi ya watu huamini pia dawa ya kikohozi ni kunywa yai bichi lililochanganywa na asali. Hizi ni imani ambazo zimejengeka kwenye jamii na watu hufanya hivyo ili kufikia malengo waliyokusudia.

Katika siku za karibuni, imevuma kuwa mayai ya kwale yanatibu magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu, saratani na kifua.

Katika mpango huo, wanapendekeza wahusika kula mayai mabichi ya kwale tena kwa kutafuna hadi kaka lake, yaani ganda la nje.

Hali hii imesababisha biashara ya mayai ya kwale kuwa kubwa na hata wafugaji wameongezeka mara dufu.

Wataalamu wanasemaje?
Baadhi ya tafiti za sayansi ya lishe na afya ya jamii, zinabainisha kuwa ulaji wa mayai katika hali ya namna ya ubichi, unaweza kuhatarisha afya.

Wakati mwingine, hali ya namna hii, huwa chanzo cha mlipuko wa magonjwa ya tumbo katika jamii. Katika milipuko ya magonjwa hayo, hali inaweza kuwa mbaya zaidi hasa kwa watoto wadogo, wazee, wajawazito na watu wenye upungufu wa kinga mwilini.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba mayai mabichi yanaweza kusababisha maradhi ya kuharisha na homa ya matumbo kutokana na kubeba vimelea vya magonjwa aina ya Salmonella Enteritidis PT4. Vimelea hivi hatari kwa afya, vinaweza kuwa ndani ya yai au juu kwenye ganda la yai bila kuonekana kwa macho. Mgonjwa aliyepata uambukizo wa bakteria wa Salmonella kutokana na kula mayai, anaweza kuwa na homa kali, maumivu makali ya tumbo pamoja na kuharisha ndani ya saa 72 baada ya kula mayai.

Ugonjwa huu unaweza kudumu kwa siku nne hadi saba na baadhi ya watu huwa na hali mbaya kiasi cha kuhitaji matibabu ya kulazwa hospitalini.

Kwa baadhi ya watu ambao kinga ya miili yao si imara, vimelea vya Salmonella vinaweza kuingia katika mfumo wa damu na kusambaa mwili mzima. Jambo hilo linaweza kusababisha kifo kwa muda mfupi kama mgonjwa hatapewa matibabu sahihi na kwa haraka.

Nchini Uingereza ingawa, ugonjwa utokanao na kula mayai yenye uambukizo wa Salmonella umepungua sana, lakini angalizo la watu kuepuka ulaji wa mayai mabichi bado linadumishwa.

“Ni swala la kujua kwamba hatari bado ipo katika jambo hili, hata kama ni ndogo,” anasema Bob Martin ambaye ni mfanyakazi wa Wakala wa Viwango vya Ubora wa Chakula (The Food Standards Agency) nchini Uingereza.

Utafiti uliofanyika mwaka 2004-2005 katika maeneo mengi ya Ulaya ulibaini kuwa asilimia 20 ya mashamba makubwa ya kuku wa mayai, yalikuwa na kuku waliokuwa na uambukizo wa Salmonella. Hii ni kwa mujibu wa Richard Lawley katika makala yake yaliyochapishwa Februari mwaka 2013 katika tovuti ya Food Safety Watch.

Utafiti mwingine uliofanywa na Q.T. Bura na Henry B. Magwisha kutoka katika Wakala wa Maabara za Mifugo Tanzania (TVLA) kwa kushirikiana na profesa Robinson H. Mdegela wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), nao ulibaini kuwa ndege wengi wanaotaga mayai wana maambukizi ya vimelea vya Salmonella. Utafiti huo ulifanyika katika Jiji la Mwanza kati ya Desemba 2013 na Januari 2014.

Tukiachilia mbali uambukizo wa Salmonella, ulaji wa muda mrefu wa mayai mabichi au yale yasiyoiva vizuri hasa kwa akina mama wajawazito, unaweza kusababisha wazae watoto wanye ulemavu wa viungo vya mwili katika maumbile yao. Utafiti wa Lawrence Sweetman na wenzake uliochapishwa mwaka 1981 katika jarida la Paediatric toleo la 68(4), unabainisha kuwa ulaji wa mayai mabichi au yasiyoiva vizuri, unaweza kusababisha watoto wasiwe na nywele kichwani.

Utafiti wa Timothy D. Durance wa Chuo Kikuu cha British Columbia nchini Canada, uliochapishwa mwaka 1991 katika jarida la Sayansi za Vyakula (Journal of Food Sciences) toleo la 56(3), unabainisha kuwa ute mweupe wa mayai unaweza kusababisha upungufu wa Biotin mwilini.

Dr. Durance anaongeza kusema kwamba, ute mweupe wa mayai mabichi una protini aina ya avidin ambayo huzuia Biotin kusharabiwa (kufyonzwa) kutoka katika chakula kinapokuwa tumboni. Utafiti huo pia ulibaini kuwa hata mayai yaliyochemshwa au kukaangwa vizuri, bado ute mweupe huwa na Avidin yenye nguvu kwa asilimia 40
Utafiti wa Profesa Hamid Said wa Chuo Kikuu cha California nchini Marekani, nao uliripoti kuwa ute wa mayai yasiyoiva, unasababisha upungufu wa Biotin mwilini. Utafiti huo ulichapishwa katika jarida la sayansi ya lishe katika tiba (American Journal of Clinical Nutrition) toleo la mwaka 2002. Utafiti mwingine ulioongozwa na Donald Mock na kuchapishwa katika jarida la sayansi ya lishe katika tiba la nchini Marekani toleo la 75(2) mwaka 2002, nao ulibainisha kuwa takribani asilimia 50 ya wanawake wajawazito, wana kiwango fulani cha upungufu wa Biotin mwilini hasa katika miezi mitatu ya mwanzo wa mimba.

Hali hii inafanya wajawazito wanaokula mayai mabichi au yasiyoiva vizuri katika kipindi hiki, kuhatarisha afya zao na za watoto wao walioko tumboni kwa kiasi kikubwa.

Utumiaji wa mayai ya namna hii kwa muda mrefu, pia unaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini na ugonjwa wa mzio wa chakula hasa kwa watoto. Lakini pia utumiaji wa mayai yasiyoiva vizuri kwa muda mrefu, unaweza kusababisha ugonjwa wa kukatika katika kwa ulimi kutokana na upungufu wa vitamini B mwilini.

Hali ambayo husababisha shida wakati wa kula vyakula vyenye uchachu au vilivyokolezwa viungo vingi vya aina mbalimbali.

Tahadhari kubwa inahitajika wakati wa kuandaa mayai ili kuhakikisha kuwa chakula hiki muhimu hakigeuki kuwa chanzo cha madhara ya kiafya. Ni vizuri kutunza, kuchagua na kusafisha mayai vizuri kabla ya kuyachemsha au kuyavunja kwa ajili ya maandalizi mbalimbali ya mapishi.

Vyombo vinavyotumika kukorogea mayai mabichi ni lazima visafishwe kwa maji ya moto na sabuni kabla ya kutumika kwa ajili ya maandalizi ya chakula. Kwa namna yoyote ile mayai yasiliwe ikiwa hayakuiva vizuri au yanapokuwa katika hali ya ubichi.

Ni wakati kwa jamii kubadili mwelekeo kwa kula mayai ambayo yamepikwa hadi kuiva na kuepuka kula yakiwa mabichi.

Ni vyema pia ikaeleweka wapikaji wanapaswa kuwaelimisha wateja wao juu ya athari hizi ili kuwafanye wawe na uchaguzi sahihi wa vyakula watakavyotumia.

Katika jamii yetu, wapika chipsi huwa hawaoshi lile bakuli la kukorogea mayai kabla hayajakaangwa. Hii ni hatari kwa sababu chombo hicho kinaweza kikawa sababu ya kusambaza maradhi kwa watumiaji wa mayai.

Home

Kingunge anusa mchezo mchafu urais ndani ya CCM

23:47

Dar es Salaam. Mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, Kingunge Ngombare Mwiru (Pichani) amesema anahisi kuna mchezo mchafu unapangwa kwenye mchakato wa kupata mgombea wa urais wa chama hicho tawala, akitaja idadi kubwa ya waliojitokeza kuwa ni ishara mbaya.

Mwanasiasa huyo mkongwe aliyefanya kazi na marais wa awamu zote nne, pia, bila kumtaja jina, alitumia muda mwingi kwenye hotuba yake kujibu kauli ya makamu mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula aliyekaririwa akisema kuwa mgombea wa chama hicho hatakiwi kujinadi.

Kingunge, ambaye amejitokeza hadharani kumpigia debe Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alionyesha hofu hiyo jana wakati mbunge huyo wa Monduli alipokuwa akihitimisha kazi ya kusaka wadhamini mkoani Dar es Salaam kwenye ofisi za CCM Mkwajuni wilayani Kinondoni.

Hadi sasa, makada waliochukua fomu kuwania urais kwa tiketi ya CCM ni 41 baada ya mwanachama mmoja kuchukua fomu jana akisema atamudu kupata wadhamini kwa njia ya mtandao katika siku tano zilizosalia. Akizungumza katika mkutano wa kusaka wadhamini ulioandaliwa kwa ajili ya Lowassa wilayani Kinondoni jana, Kingunge alipingana na kauli ya Mangula kuwa mgombea wa CCM atanadiwa na chama, si kujinadi mwenyewe akisema chama hicho kinataka mgombea anayekubalika ndani na nje.

Siku tatu zilizopita, Mangula alihojiwa na kituo cha televisheni cha Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) na kusema mgombea wa chama hicho hatakiwi kujinadi mwenyewe, kusisitiza kuwa anatakiwa kunadiwa na chama.

Lakini Kingunge aliikosoa kauli hiyo jana akisema chama hicho kimeweka utaratibu na hakuna sababu ya kuuacha na kuanza kuwahukumu wagombea kabla ya vikao na kusisitiza kuwa CCM haikuwahi kuwahukumu wagombea kabla katika chaguzi zilizopita.

“Mchakato ufuate taratibu zilizowekwa,” alisema Kingunge ambaye aliibuka Kinondoni ambako Lowassa alimalizia shughuli zake jijini Dar es Salaam.

“Nimemsikia kiongozi wetu mmoja tena juzi juzi hapa, nikamuona kwenye televisheni anasema mtu hawezi kwenda kujinadi yeye binafsi, ananadiwa na chama.

“Nikasema eh! hilo hilo. Lakini nataka nimweleze yeye na wenye fikra kama hizo kuwa kuna ngazi mbili katika utaratibu wetu; kwanza, mwanachama anayetaka kuwania ubunge, udiwani, urais lazima ajinadi ndani ya chama, ndivyo tulivyofanya miaka yote kwa mujibu wa katiba na taratibu zetu. Ndivyo wanavyofanya sasa wakina Lowassa.”

Alisema pili, wagombea wakishajinadi chama kitamteua mmoja ambaye kitamnadi na yeye ataendelea kujinadi.

“Si vizuri watu ambao tumewapa vyeo katika chama wakaanza ama wakaendelea kukitumia chama chetu kwa mambo yao binafsi. Kama wana mashaka tupo tunaojua mambo ya chama,” alisema Kingunge huku akishangiliwa na mamia ya watu.

Kingunge alisema mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa Dodoma alisema chama kinatafuta mgombea anayekubalika ndani na nje ya chama hicho ili kuweza kushindana na vyama vingine










Home

BREAKING NEWS: WATU WATATU WAUAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI

07:26

Watu watatu wamefariki wawili kati yao wanasadikiwa kuwa ni wafuasi wa Al shabaab katika mapigano baina yao na polisi 

Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro amesema tukio hilo limetokea eneo la mpakani mwa mkoa wa Morogoro na wilaya ya mvomero na mkoa wa Tanga ambapo watu wao walikuwa wamejificha msituni 
amesema jeshi hilo linawashikilia watu sita kwa kuhusika na tukio hilo, na kwamba  uchunguzi zaidi unafanyikanikiwa ni pamoja na msako mkali katika eneo hilo

Taarifa kutoka katika hospitali ya mission ta turiani mkoani morogoro zinasema kuwa maiti tatu zimehifadhiwa hapo kati ya hizo, mbili zinaonekana si za raia kutoka Tanzania huku moja ikiwa ni ya mtu aliyekuwa amejeruhiwa vibaya na baadaye kufariki akiwa hospitalini hapo.

Home

POLISI AUWA NA MAJAMBAZI, YAIBA MAMILIONI NMB MKURANGA

06:28

Majambazi watatu, wakiwa na silaha aina ya SMG, jana asubuhi waliua askari mmoja na kujeruhi watu wengine wawili na baadaye kupora bunduki na mamilioni ya fedha kwenye benki ya NMB, Tawi la Mkuranga  mkoani hapa.

Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya gari kuwasili na makasha ya fedha, huku shughuli za utoaji huduma kwenye tawi hilo zikiendelea.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Pwani, Jafar Ibrahimu alisema kuwa bado hajafahamu kiasi halisi cha fedha zilizoporwa kwani alikuwa hajafika eneo la tukio.

Hata hivyo alisema askari aliyeuawa hakuwa mmoja wa polisi waliokuwa lindo kwenye tawi hilo la NMB, bali alikuwa anapita kuelekea kazini ndipo akakumbana na tukio hilo

Kamanda Ibrahim alibainisha kuwa taarifa ya awali aliyonayo ni kwamba katika tukio hilo hakuna silaha wala risasi iliyoporwa na majambazi hayo.

“Ndio ninakwenda eneo la tukio, kwani awali ninaweza kusema kweli tukio la ujambazi limetokea hapo NMB na nimeelezwa kuna askari kauawa, lakini si mmoja wa wale waliokuwapo lindoni,” alisema Kamanda Ibrahim.

“Lakini pia hakuna silaha iliyoporwa, zilizochukuliwa ni fedha ambazo bado haijafahamia ni kiasi gani na ziliporwa zikiwa tayari zimefikishwa ndani ya ofisi hiyo. Askari waliokuwa wamezisindikiza siyo polisi wetu bali ni wa kampuni binafsi,” alisema Kamanda Ibrahim.

Alisema kwa sasa, polisi wa  Wilaya ya Mkuranga, Rufiji na Dar es Salaam wapo katika msako mkali kuwasaka watu waliohusika katika tukio hilo la ujambazi.

Akizungumzia tukio hilo, mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Abdalah Kihato alisema majambazi hao waliokuwa watatu walivamia benki wakati wafanyakazi wa benki hiyo wakiwa katika maandalizi ya kupokea fedha hizo.

“Inaonekana majambazi hao walikuwa na taarifa za ujio wa fedha hizo kwenye benki hiyo,” alisema.

Alisema polisi mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi, na kwa mujibu wa Kihato, polisi huyo alikuwa akijiandaa kuingia kazini jana mchana, huku askari wawili waliokuwa zamu kituoni hapo  wakijeruhiwa kwa risasi.

Mwingine aliyejeruhiwa ni mtumishi mmoja wa benki hiyo ambaye alipigwa panga. Wote wamehamishwa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga kwa matibabu.
Alisema baada ya tukio hilo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ilikutana kwa dharura kulijadili kwa kina na kwamba kwa sasa polisi pamoja na timu ya ulinzi na usalama ya wilaya iko kazini kutafuta taarifa zaidi za tukio hilo.

 Alipoulizwa iwapo uporaji wa fedha hizo ulifanikiwa kutokana na uzembe, Kihato alisema kuwa uchunguzi wa polisi unaendelea.

Kihato aliwaomba wananchi wa Mkuranga na wale wa jiji la Dar es Salaam kutoa ushirikiano kwa polisi ili kufanikisha kukamatwa kwa wezi hao ambao alisema wameonyesha unyama wa hali ya juu.

 Hata hivyo, chanzo cha habari kilidai kuwa polisi aliyeuawa alipigwa risasi wakati akitoka ndani ya benki ambamo alikwenda kupata huduma.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, majambazi watatu kati yatisa walifika hapo wakiwa kwenye pikipiki na walshuka na kuelekea kwenye mlango wa kuingilia ndani na kuingia kama wateja wengine.

Dakika kadhaa baada ya watu hao watatu kuingia ndani, walitoa silaha na kuwataka wote waliokuwamo ndani kusikiliza maelekezo na kwamba ambaye angekaidi angefumuliwa ubongo.

Mashuhuda hao walidai kuwa wateja walitii amri hiyo na ghafla ulisikika mlio wa risasi nje ya benki hiyo kisha mmoja wa majambazi alitoka na sanduku lililokuwa na fedha na akalipasua nje ya benki na kutoa fedha na kuziingiza kwenye mifuko mikubwa ya plastiki na kuondoka nazo kwa pikipiki waliokuja nayo.

Mlio ule wa risasi iliyosikika nje ya benki inadaiwa ilitoka kwa mmoja wa majambazi wengine ambao wao walikuja na gari dogo na kugawanyika wao wakabaki kufuatilia nyenendo za polisi waliokuwa zamu eneo hilo na askari wawili wa kampuni binafsi waliokuwa wamesindkiza fedha hizo zilipokuwa zimeshushwa kutoka kwenye gari na kuingizwa ndani ya ofisi. Imeelezwa kuwa majambazi hao waliokuwa nje askari aliyekuwa amevaa kiraia akiingia benki na akawa anafanya mawasiliano fulani, kitendo ambacho walihisi anatoa taarifa kwa wenzake na hivyo wakaamua kumuwahi kwa risasi ya kichwani.

  • Kiasi halisi cha fedha zilizoibiwa bado hakijafahamika.
  • Kwa sasa polisi wa  Wilaya ya Mkuranga, Rufiji na Dar es Salaam wapo katika msako mkali kuwasaka watu waliohusika katika tukio hilo la ujambazi


TujikumbusheJuni 11 mwaka huu, majambazi walivamia kituo cha polisi cha Mkuranga wakiwa na mapanga na kuua askari mmoja na kisha kupora bunduki mbili.

Home

CCM YAITISHA KAMATI KUU KWA DHARURA

02:05

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete ameitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu (CC) kitakachofanyika mjini Dodoma, huku ajenda kuu ikiwa ni kupitisha majina ya wagombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), zilizo wazi kutokana na sababu mbalimbali.
Kitengo cha Mawasiliano cha CCM kimethibitisha uwapo wa kikao hicho ambacho pia kitapitia orodha ya makada wa chama hicho wanaowania urais.
Kikao hicho kitatanguliwa na kikao kingine cha sekretarieti kinachofanyika leo ambacho kitaongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana. Mpaka sasa, makada 40 wamejitokeza kuomba nafasi ya kuipeperusha bendera ya CCM katika kiti cha urais, kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, wengi wanaendelea na kazi ya kukusanya wadhamini katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Juzi, wakati akizungumza na Televisheni ya Taifa (TBC), Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara, Philip Mangula aligusia kidogo juu ya wagombea urais na kusema atakayepitishwa hatajiuza mwenyewe, bali atauzwa na chama hicho alichodai kuwa kina wanachama milioni saba nchi nzima.
Chama hicho tawala kinakabiliwa na wakati mgumu wa kupitisha jina la mgombea urais kutokana na idadi kubwa ya waliojitokeza kuwania nafasi hiyo jambo ambalo halikujitokeza wakati wa upitishwaji wa mgombea urais wa chama hicho mwaka 1995 na 2005.
Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa huenda kikao hicho kikahudhuriwa na wajumbe wachache kutokana na kuitishwa kwa dharura.
Ilieleza kuwa kuna nafasi zilizo wazi kutokana na sababu mbalimbali, kuanzia ngazi za wilaya mpaka taifa na kwamba lazima zijazwe katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ili kila mtu atimize wajibu wake.
 “Kuna nafasi za makatibu na wenyeviti ambazo ziko wazi kuanzia wilayani mpaka taifa. Kikao hicho kinakwenda kuzibainisha na kisha kuzijaza,” kilieleza chanzo hicho.
Suala jingine litakalojadiliwa katika kikao hicho ni mabadiliko ya uongozi katika nafasi ya Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Uhuru, Joseph Kulangwa ambayo imesababisha mgomo wa wafanyakazi wanaopinga uamuzi huo. Gazeti hilo ni la chama hicho tawala.
Kwa mujibu wa ratiba ya chama hicho, Kamati ya Usalama na Maadili itafanya kikao chake Julai 8 na kufuatiwa na Kamati Kuu Julai 9 ambayo inatarajiwa kuchuja wagombea hao 40 na kupata watano ambao majina yao yatawasilishwa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) itakayofanyika Julai 10 kuchuja wagombea hao na kubaki watatu watakaopigiwa kura na mkutano mkuu kumpata mmoja. Mkutano huo mkuu utafanyika Julai 11 na 12 .

Home

mtu mmoja achinjwa ufaransa

11:50


Mtu mmoja amechinjwa na mwengine akajeruhiwa vibaya baada ya shambulizi la kiislamu katika mji wa Lyon Ufaransa.
Vilipuzi kadhaa vilitegwa katika karakana moja iliyoko Saint-Quentin-Fallavie
Mwanaume mmoja amekamatwa na maafisa wa usalama kufuatia tukio hilo
Mvamizi aliyetekeleza mauaji hayo anasemekana kuwa alikuwa akipeperusha kibendera cha wanamgambo wa kiislamu.
Kibendera hicho kilipatikana kimetupwa karibu na eneo la tukio.
Inaaminika kuwa waliotekeleza shambulizi hao walikuwa na bendera iliyoandikwa katika kiarabu
Mwanaume mmoja amekamatwa na maafisa wa usalama kufuatia tukio hilo.
Waziri wa usalama wa ndani Bernard Cazeneuve yuko njiani kuelekea kwenye eneo la tukio.


Hili ni shambulizi la kwanza tangu watu 17 wauawe miezi sita iliyopita

Wakati huohuo rais wa Ufaransa Francois Hollande anatarajiwa kukatiza ziara yake rasmi ya viongozi wa bara ulaya na kurejea nyumbani kukabili janga hilo.
Shambulizi hili ni la kwanza tangu lile la kigaidi lililopelekea kuuawa kwa watu 17 miezi sita iliyopita

Education

slave trade in Africa, factor for and its effect in Africa and other continent

04:22

Slavery is the ownership and control of one human being by another or we can say slavery is legal or economic system under which people are treated as property where by slave may be bought and sold and can be held slave from the time of their capture[1] .
Triangular slave trade usually is historical posts or regional triangular trade usually involve when regions from which its major import come. Triangular this was the trade between three continents such as America, Africa, and Europe where by trade cross the Atlantic Ocean, this trade emerged during the 16th up to the 19th[2].
An Atlantic slave in Africa began in 1444, when the Portuguese began to ship slaves from west Africa to America for the next hundred years the main market for these slaves were Europe and the Atlantic islands owned by Portugal and Spain. However, the discovery of the America in 1492 by Christopher Columbus led to the creation of new colonies with great need for cheap labor, and in the mid-sixteenth century the European ship were carrying African slaves to Brazil, the Caribbean islands and North America in steady of increase production.
Triangular slave trade operate where by European ship carried European manufactured goods to Africa such as sugar, mirrors, clothes, bears and other luxury goods and exchange them for slave, these slaves were then taken to America whereby they were traded for sugar, cotton, tobacco, and they are used as are workers in plantations, and other domestic works in America and others were transported to Europe. It is estimated that, between sixteenth and nineteenth centuries over twelve millions Africans were transported across the Atlantic most of them come from West Africa the regional origins of the enslaved population in Africa are. The enslaved population came from all parts of the Atlantic coast of Africa, from Senegambia to southern Angola, and some enslaved people came from southeastern Africa, especially in Sierra Leone, Windward Coast. Gold Coast, Bight of Benin, Bight of Biafra, West Central and South East Africa this is especially in the nineteenth century. Tran’s triangular slave trade is divided into two areas known as the first and second Atlantic system.
First Atlantic was the trade of slaved African to primarily south America colonial of the Portuguese and Spanish empires it accrued for only  slightly  more than 3% of all Atlantic slave trade it started  on significance  in about  1502 and lasted 1580  when Portugal was temporally   united  with Spain  while Portuguese  traded  enslave people  themselves  the Spanish essential system  during the first Atlantic[3] system traders  were Portuguese giving The Portuguese dominated the first period. Some slaves were moved along the shores of western Africa, for retention and use within Africa and some were taken to Portugal and Spain. Already by the 1490s, before Columbus reached the Caribbean, the Portuguese established sugar plantations using enslaved labor on a scale that foreshadowed the development of plantation slavery in the Americas. Enslaved Africans were already being taken to the Americas; they were part of every expedition into the regions that became the Spanish colonies, and after the 1540s they were taken to Portuguese Brazil to grow sugar[4].
Second Atlantic system  was the trade  of enslaved  by mostly British, Portuguese, Brazilian ,French and Dutch traders the main destination of this phase were the Caribbean colonies Brazil  and America a number  European countries  built up economically slave dependent Colonies  in the new world  amongst the properties of this system where frays drake and john hasten Also the following are the society participated in the Atlantic slave trade there is Ghana where there is Asante confederacy and mankessim kingdom, Sierra leone-koyatemne, Benin such as kingdom of dahomey, Guinea there is kingdom foutadyall on the final period of the transatlantic trade in humans lasted until the 1860s[5]. In this period, Brazil, Cuba, and Puerto Rico were the principal destinations for enslaved Africans, since slaves could no longer legally be brought into North America, British or French colonies in the Caribbean, or the independent countries of Spanish America. Similarly, on the African side most slaves were traded in only a few ports such as Luanda in Angola, Ouidah (Whydah) in the Bight of Benin, Bonny in the Bight of Biafra, and the adjacent trade “castles” at Koromatin and Winneba on the Gold Coast; these port they stand out as the points of departure for the greatest number of enslaved Africans bound for the Americas; these points probably accounted for at least one-third of all Africans sent to the Americas. Other major ports included Old Calabar in the Bight of Biafra; Benguela in southern Angola; Cabinda, to the north of the Congo River; and Lagos, in the Bight of Benin in the nineteenth century[6] after see short about the history of Atlantic slave trade now let look on the Contribution of Africa to the development and consolidation triangular slave trade as follows;
Source of labor; the African  were taken  as slave  which were highly needed  in the America  as labor in plantation production  which produce raw material which were  highly needed  for the industries  for example  plantation  which was established  in America for example of the plantation  which was established in America  are sisal plantation ,sugar plantation and cotton plantation which needed labor for the plantation  of raw material which were  needed  in industrial, African labor were needed in whites plantation in America because the American and European were lazy and they are not  physically feat hence they need African labor for the production[7]. During that period Portuguese and Spain were the possessor of the majorly America tropical colonies were not in the position to provide workers and the solution was to take Africans as the source of production. In North America and elsewhere in the Americas, the use of terror was basic to this mechanism of labor supply .Africans went to areas that were developing economically, often leaving in their wake areas of economic dislocation and desolation. North America was typical in this regard, since African slave labor was central to several of the most important colonies, particularly South Carolina, Virginia, and Maryland and, indirectly, through commerce in other colonies, such as Massachusetts, New York, and Pennsylvania.
Source of markets African acted as source of markets for European  finished  goods where after  European  manufactured  goods were  imported to Africa were  they sell their goods  to Africans  hence  they get  high profit  for example Timbuktu and Gao they was their the goods market for European surplus goods[8].
Africa as a source  of raw material  Africa they acted as source of raw material which were  highly  needed  in the  industrial  such as gold and silver  were taken from Africa  and which were taken by European to Africa which they need to made ornament and then where return for Africa[9].
Africa trader  and chiefs also contribute  to the development of triangular slave trade  whereby they  are the ones  who conquer  or capture  their fellow  Africans then sell them to the European slave trader dealer  on selling  their fellow  they get  luxury goods  such glasses, clothes, on doing  so they contribute to the development of triangular slave trade, the means in which the slaves were obtained was through the selling the culprits who were the criminal also they going village after village ambush them or raid the people and when they get them they sell them as slaves, also the prisoner of the war they was also sold as slaves, another means was through trickery and kidnapping[10] wherever they found people who have the ability to become a slave and they can gain much profit also these African chiefs they play another role whereby they guide the European or Arab’s slave raider into the village in which they can obtain slaves, also they hand over the wrong doers from their societies to the slave trader[11]in return they get luxury’s goods, by doing so Atlantic slave trade continue to grow and many of African also shipped to America as slave because of things done by Africans slave trader and African chiefs.
Also Africans  played a big role  in triangular slave trade,  this was through  the issues of investment which was done in African nations this means that European were using  African land  for production  of raw material  such as Comoros islands were by European they produce their raw material then they ship them to the Europe or America were they can be processed and become finished good and then , the surplus they brought to Africa and sold at high price while they are the ones who use their power to make sure they become raw material.
Generally the African societies contributes the developments triangular slave trade become they provide raw material which were highly needed in the industries for the manufacturing and also provide a labor for the plantation which were highly needed in the production
REFERENCES
Adediran, B. (1984). Yoruba Ethnic Groups or a Yoruba Ethnic Group A Review of the Problem of Ethnic Identification, vol. 7. Africa: USP.
Behrendt & Stephen D. (1993).The British slave trade, 1785–180 its profitability, and
mortality. Wisconsin: University of Wisconsin.
Clarkson, T.  (1785). Essay on the Inhumanity of the Slave Trade. Cambridge: Cambridge
University.
Colclanis, and Peter A.  (2005).the Atlantic Economy during the Seventeenth and Eighteenth
Centuries: Organization, Operation, Practice, and Personnel. Columbia: University of South Carolina Press.
Curtin, P. D. (1967). Africa Remembered: Narratives by West Africans from the Era of the
Slave Trade. Madison: University of Wisconsin Press.
Curto, C. and Paul E. (2004).Enslaving Spirits at Luanda. Netherlands: Hinterland Leiden.
Dantzig, A. (1975). Effect of the Atlantic Slave Trade on Some West African Societies.
Netherlands: Hinterland Leiden.
Eltis, D. (1992). Was the Slave Trade Dominated by Men?”Journal of Interdisciplinary
History, vol. 23.Cambridge England: Cambridge University Press.
Eltis, D. (2000).The Rise of African Slavery in the Americas, Cambridge England: Cambridge University Press.




[1]Clarkson, T.  (1785). “Essay on the Inhumanity of the Slave Trade”. Cambridge: Cambridge University. Pp. 5
[2]Behrendt & Stephen D. (1993).The British slave trade, 1785–1807, profitability, and mortality. Wisconsin: University of Wisconsin. Pp 12
[3]Colclanis, and Peter A.  (2005). the Atlantic Economy during the Seventeenth and Eighteenth Centuries: Organization, Operation, Practice, and Personnel. Columbia: University of South Carolina Press. Pp. 45-46
[4]ibd
[5]Curtin, P. D. (1967). Africa Remembered: Narratives by West Africans from the Era of the Slave Trade, Madison, WI: University of Wisconsin Press.
[6]Colclanis, and Peter A.  (2005). The Atlantic Economy during the Seventeenth and Eighteenth Centuries: Organization, Operation, Practice, and Personnel. Columbia: University of South Carolina Press.
[7]Clarkson, T.  (1785). “Essay on the Inhumanity of the Slave Trade”. Cambridge: Cambridge University                                                      Press
[8]Dantzig, A. (1975). Effect of the Atlantic Slave Trade on Some West African Societies. Netherlands: Hinterland Leiden, pp. 252–269.
[9]ibd
[10]Curto, C. and Paul E. (2004).Enslaving Spirits at Luanda. Netherlands: Hinterland Leiden. pp. 134
[11]Eltis, D. (1992). Was the Slave Trade Dominated by Men?”Journal of Interdisciplinary History, vol. 23.                  Cambridge England: Cambridge University Press. pg. 237–257.

Home

Kutoka Bungeni: Sugu anajibu tuhuma za kupora mtoto kutoka kwa mzazi mwenzake

03:37


  1. Baada ya jana Martha Mlata
    kumtuhumu Sugu kumpora mtoto 
    toka kwa mama yake. 
    amemuomba Spika kutoa maelezo binafsi. 
    Kwanza anakiri mtoto ni wake, 
    na anasema watu wazima 
    hawazungumzii mambo ya ndoa za wenzake 
    na anasema ni mambo binafsi.


    Anasema binti yake ameishi Dar
    tangu mwaka 2012 
    na amekuwa akilipa laki tano kila mwezi 
    na mi 3 kwa mwaka kama karo.

    Anasema mzazi mwenzake amekuwa 
    akivaa nusu uchi na 

    kuachasehemu za siri nje.
    Anasema Mlata anayejiita mlokole 
    hawezi kutetea maovu kama hayo, 
    na yeye hasemi kwa nini ndoa yake 

    ilivunjika .
    Anasema kile kinachodaiwa kuwa 
    kumpora mtoto ni hukumu ya mahakama
    na Mlata hakuwa shaidi wala hana uhakika 

    kama hata mtoto mwenyewe anamjua.

    Anasema kwa kuwa ni mambo ya faragha 
    hata Mlata asingetaka mambo 

    yake na mabwana zake wa sasa yajulikane.

    Anasema hata mtoto hajamchukua 
    na ameacha maswala ya kifamilia 

    yachukue mkondo wake.

    Ndugai anasema suala hili liachwe 
    maana linaweza kumuathiri mtoto 
    kisaikolojia hata shule.
    Anawataka waandishi wa habari kuliacha suala hili.  
    MH. J. mbilinyi
    Sugu anatokwa na machozi kwa uchungu

Like us on Facebook

About me

Ismail mbaazi
Email: mbaazishumaa6@gmail.com
#+25565-9230-273