ISLAMIC STATE WATHIBITISHA JIHAD JOHN ALIUAWA

23:38


JohnImage copyrighP
Image captionJihadi John alitumiwa sana katika video za propaganda za IS
Kundi la Islamic State limethibitisha kwamba mwanamgambo aliyetafutwa sana na mataifa ya Magharibi, aliyejulikana kama Jihadi John, alifariki.
Kundi hilo limetangaza kifo chake kwenye jarida lake la mtandaoni kwa jina Dabiq.
Mwanamgambo huyo aliuawa kwenye shambulio lililotekelezwa kwa kutumia ndege isiyokuwa na rubani Novemba mwaka jana.
Marekani, baada ya kutekeleza shambulio hilo katika ngome ya IS mjini Raqqa, ilisema ilikuwa na “uhakika kiasi” kwamba alikuwa ameuawa.
Mwingereza huyo, ambaye jina lake la kuzaliwa ni Mohammed Emwazi, alionekana kwenye video nyingi za IS akiwakata shingo mateka kutoka mataifa ya Magharibi wakiwemo Waingereza David Haines, aliyekuwa mfanyakazi wa shirika la kutoa misaada, na dereva wa teksi Alan Henning.
Kwenye tangazo la tanzia kwenye jarida hilo, Emwazi anaitwa Abu Muharib al-Muhajir, jina alilojulikana nalo katika kundi hilo.
Maelezo ya kifo chake yanathibitisha taarifa kutoka kwa Marekani kuhusu yaliyotokea siku hiyo.
Kundi hilo limesema Emwazi aliuawa tarehe 12 Novemba “gari alimokuwa akisafiria liliposhambuliwa na ndege isiyo na rubani katika mji wa Raqqa, ambapo gari lake liliharibiwa na akafariki papo hapo.”
Picha ya mwanamgambo huyo akiwa ametabasamu, na ambaye anaonekana akiwa hajajifunika uso huku akiwa ameangalia chini, imechapishwa kwenye jarida hilo.
Emwazi alizaliwa nchini Kuwait mwaka 1988 lakini akahamia Uingereza mwaka 1994 akiwa na umri wa miaka sita.

Watu wenye silaha wavamia chuo kikuu Pakistan

23:35


Watu wenye silaha wameshambulia chuo kikuu kimoja eneo la Charsadda kaskazini magharibi mwa Pakistan.
Washambuliaji walijaribu kuingia ndani ya chuo kikuu cha Bacha Khan kwa nguvu na makabiliano kati yao na maafisa wa usalama bado yanaendelea, ripoti zinasema.
Milipuko miwili mikubwa imesikika, afisa wa polisi ameambia shirika la habari la Reuters.
Ripoti zinasema watu wawili wamejeruhiwa. Maafisa wa usalama wamezingira chuo kikuu hicho.
Eneo la Charsadda liko umbali wa kilomita 50 (maili 30) kutoka jiji la Peshawar, ambako wapiganaji wa Taliban waliua zaidi ya wanafunzi 130 baada ya kushambulia shule moja.

Mwanamume mzee zaidi duniani afariki Japan

09:52


YasutaroImage copyrightGetty
Image captionYasutaro alizaliwa Machi 1903
Mwanamume mkongwe zaidi duniani amefariki nchini Japan akiwa na umri wa miaka 112.
Yasutaro Koide, kutoka jiji la Nagoya, alizaliwa tarehe 13 Machi 1903 na alifanya kazi kama fundi wa nguo wakati wa ujana wake.
Alitambuliwa na Guiness Book of World Records kama mwanamume mzee zaidi duniani Agosti mwaka jana.
Yasutaro alifariki kutokana na maradhi ya moyo na nimonia mapema Jumanne.
Alipoulizwa kuhusu siri ya maisha marefu alipokuwa hai, anadaiwa kuwashauri watu waache kujiumiza sana na kazi na pia waishi kwa furaha.
Kwa sasa mtu mkongwe zaidi duniani ni Mwamerika, Susannah Mushatt Jones, ambaye ana umri wa miaka 116.
Alichukua nafasi hiyo mwaka jana baada ya kifo cha Misao Okawa kutoka Japan aliyekuwa na umri wa miaka 117.
Mtu aliyeishi muda mrefu zaidi duniani kwa mujibu wa Guinness alikuwa Mfaransa Jeanne Calment, aliyeishi miaka 122 na siku 164. Alifariki Agosti 1997

Like us on Facebook

About me

Ismail mbaazi
Email: mbaazishumaa6@gmail.com
#+25565-9230-273