Home

BREAKING NEWS: WATU WATATU WAUAWA KATIKA MAPAMBANO NA POLISI

07:26

Watu watatu wamefariki wawili kati yao wanasadikiwa kuwa ni wafuasi wa Al shabaab katika mapigano baina yao na polisi 

Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro amesema tukio hilo limetokea eneo la mpakani mwa mkoa wa Morogoro na wilaya ya mvomero na mkoa wa Tanga ambapo watu wao walikuwa wamejificha msituni 
amesema jeshi hilo linawashikilia watu sita kwa kuhusika na tukio hilo, na kwamba  uchunguzi zaidi unafanyikanikiwa ni pamoja na msako mkali katika eneo hilo

Taarifa kutoka katika hospitali ya mission ta turiani mkoani morogoro zinasema kuwa maiti tatu zimehifadhiwa hapo kati ya hizo, mbili zinaonekana si za raia kutoka Tanzania huku moja ikiwa ni ya mtu aliyekuwa amejeruhiwa vibaya na baadaye kufariki akiwa hospitalini hapo.

Home

POLISI AUWA NA MAJAMBAZI, YAIBA MAMILIONI NMB MKURANGA

06:28

Majambazi watatu, wakiwa na silaha aina ya SMG, jana asubuhi waliua askari mmoja na kujeruhi watu wengine wawili na baadaye kupora bunduki na mamilioni ya fedha kwenye benki ya NMB, Tawi la Mkuranga  mkoani hapa.

Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya gari kuwasili na makasha ya fedha, huku shughuli za utoaji huduma kwenye tawi hilo zikiendelea.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Pwani, Jafar Ibrahimu alisema kuwa bado hajafahamu kiasi halisi cha fedha zilizoporwa kwani alikuwa hajafika eneo la tukio.

Hata hivyo alisema askari aliyeuawa hakuwa mmoja wa polisi waliokuwa lindo kwenye tawi hilo la NMB, bali alikuwa anapita kuelekea kazini ndipo akakumbana na tukio hilo

Kamanda Ibrahim alibainisha kuwa taarifa ya awali aliyonayo ni kwamba katika tukio hilo hakuna silaha wala risasi iliyoporwa na majambazi hayo.

“Ndio ninakwenda eneo la tukio, kwani awali ninaweza kusema kweli tukio la ujambazi limetokea hapo NMB na nimeelezwa kuna askari kauawa, lakini si mmoja wa wale waliokuwapo lindoni,” alisema Kamanda Ibrahim.

“Lakini pia hakuna silaha iliyoporwa, zilizochukuliwa ni fedha ambazo bado haijafahamia ni kiasi gani na ziliporwa zikiwa tayari zimefikishwa ndani ya ofisi hiyo. Askari waliokuwa wamezisindikiza siyo polisi wetu bali ni wa kampuni binafsi,” alisema Kamanda Ibrahim.

Alisema kwa sasa, polisi wa  Wilaya ya Mkuranga, Rufiji na Dar es Salaam wapo katika msako mkali kuwasaka watu waliohusika katika tukio hilo la ujambazi.

Akizungumzia tukio hilo, mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Abdalah Kihato alisema majambazi hao waliokuwa watatu walivamia benki wakati wafanyakazi wa benki hiyo wakiwa katika maandalizi ya kupokea fedha hizo.

“Inaonekana majambazi hao walikuwa na taarifa za ujio wa fedha hizo kwenye benki hiyo,” alisema.

Alisema polisi mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi, na kwa mujibu wa Kihato, polisi huyo alikuwa akijiandaa kuingia kazini jana mchana, huku askari wawili waliokuwa zamu kituoni hapo  wakijeruhiwa kwa risasi.

Mwingine aliyejeruhiwa ni mtumishi mmoja wa benki hiyo ambaye alipigwa panga. Wote wamehamishwa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga kwa matibabu.
Alisema baada ya tukio hilo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ilikutana kwa dharura kulijadili kwa kina na kwamba kwa sasa polisi pamoja na timu ya ulinzi na usalama ya wilaya iko kazini kutafuta taarifa zaidi za tukio hilo.

 Alipoulizwa iwapo uporaji wa fedha hizo ulifanikiwa kutokana na uzembe, Kihato alisema kuwa uchunguzi wa polisi unaendelea.

Kihato aliwaomba wananchi wa Mkuranga na wale wa jiji la Dar es Salaam kutoa ushirikiano kwa polisi ili kufanikisha kukamatwa kwa wezi hao ambao alisema wameonyesha unyama wa hali ya juu.

 Hata hivyo, chanzo cha habari kilidai kuwa polisi aliyeuawa alipigwa risasi wakati akitoka ndani ya benki ambamo alikwenda kupata huduma.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, majambazi watatu kati yatisa walifika hapo wakiwa kwenye pikipiki na walshuka na kuelekea kwenye mlango wa kuingilia ndani na kuingia kama wateja wengine.

Dakika kadhaa baada ya watu hao watatu kuingia ndani, walitoa silaha na kuwataka wote waliokuwamo ndani kusikiliza maelekezo na kwamba ambaye angekaidi angefumuliwa ubongo.

Mashuhuda hao walidai kuwa wateja walitii amri hiyo na ghafla ulisikika mlio wa risasi nje ya benki hiyo kisha mmoja wa majambazi alitoka na sanduku lililokuwa na fedha na akalipasua nje ya benki na kutoa fedha na kuziingiza kwenye mifuko mikubwa ya plastiki na kuondoka nazo kwa pikipiki waliokuja nayo.

Mlio ule wa risasi iliyosikika nje ya benki inadaiwa ilitoka kwa mmoja wa majambazi wengine ambao wao walikuja na gari dogo na kugawanyika wao wakabaki kufuatilia nyenendo za polisi waliokuwa zamu eneo hilo na askari wawili wa kampuni binafsi waliokuwa wamesindkiza fedha hizo zilipokuwa zimeshushwa kutoka kwenye gari na kuingizwa ndani ya ofisi. Imeelezwa kuwa majambazi hao waliokuwa nje askari aliyekuwa amevaa kiraia akiingia benki na akawa anafanya mawasiliano fulani, kitendo ambacho walihisi anatoa taarifa kwa wenzake na hivyo wakaamua kumuwahi kwa risasi ya kichwani.

  • Kiasi halisi cha fedha zilizoibiwa bado hakijafahamika.
  • Kwa sasa polisi wa  Wilaya ya Mkuranga, Rufiji na Dar es Salaam wapo katika msako mkali kuwasaka watu waliohusika katika tukio hilo la ujambazi


Tujikumbushe; Juni 11 mwaka huu, majambazi walivamia kituo cha polisi cha Mkuranga wakiwa na mapanga na kuua askari mmoja na kisha kupora bunduki mbili.

Home

CCM YAITISHA KAMATI KUU KWA DHARURA

02:05

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete ameitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu (CC) kitakachofanyika mjini Dodoma, huku ajenda kuu ikiwa ni kupitisha majina ya wagombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), zilizo wazi kutokana na sababu mbalimbali.
Kitengo cha Mawasiliano cha CCM kimethibitisha uwapo wa kikao hicho ambacho pia kitapitia orodha ya makada wa chama hicho wanaowania urais.
Kikao hicho kitatanguliwa na kikao kingine cha sekretarieti kinachofanyika leo ambacho kitaongozwa na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana. Mpaka sasa, makada 40 wamejitokeza kuomba nafasi ya kuipeperusha bendera ya CCM katika kiti cha urais, kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, wengi wanaendelea na kazi ya kukusanya wadhamini katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Juzi, wakati akizungumza na Televisheni ya Taifa (TBC), Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara, Philip Mangula aligusia kidogo juu ya wagombea urais na kusema atakayepitishwa hatajiuza mwenyewe, bali atauzwa na chama hicho alichodai kuwa kina wanachama milioni saba nchi nzima.
Chama hicho tawala kinakabiliwa na wakati mgumu wa kupitisha jina la mgombea urais kutokana na idadi kubwa ya waliojitokeza kuwania nafasi hiyo jambo ambalo halikujitokeza wakati wa upitishwaji wa mgombea urais wa chama hicho mwaka 1995 na 2005.
Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa huenda kikao hicho kikahudhuriwa na wajumbe wachache kutokana na kuitishwa kwa dharura.
Ilieleza kuwa kuna nafasi zilizo wazi kutokana na sababu mbalimbali, kuanzia ngazi za wilaya mpaka taifa na kwamba lazima zijazwe katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ili kila mtu atimize wajibu wake.
 “Kuna nafasi za makatibu na wenyeviti ambazo ziko wazi kuanzia wilayani mpaka taifa. Kikao hicho kinakwenda kuzibainisha na kisha kuzijaza,” kilieleza chanzo hicho.
Suala jingine litakalojadiliwa katika kikao hicho ni mabadiliko ya uongozi katika nafasi ya Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Uhuru, Joseph Kulangwa ambayo imesababisha mgomo wa wafanyakazi wanaopinga uamuzi huo. Gazeti hilo ni la chama hicho tawala.
Kwa mujibu wa ratiba ya chama hicho, Kamati ya Usalama na Maadili itafanya kikao chake Julai 8 na kufuatiwa na Kamati Kuu Julai 9 ambayo inatarajiwa kuchuja wagombea hao 40 na kupata watano ambao majina yao yatawasilishwa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) itakayofanyika Julai 10 kuchuja wagombea hao na kubaki watatu watakaopigiwa kura na mkutano mkuu kumpata mmoja. Mkutano huo mkuu utafanyika Julai 11 na 12 .

Like us on Facebook

About me

Ismail mbaazi
Email: mbaazishumaa6@gmail.com
#+25565-9230-273