ujasiriamali November 2016 - UJASIRIAMALI
Education

Moja ya kesi zilizokuwa Ngumu,Gumzo na ya Kihistoria Duniani

08:04

Kwa wale ambao wamekuwa wakifuatilia kwa ukaribu yale yanayotokea nchi za wenzetu hasa Marekani na Visa na Mikasa ya matajiri. watu maarufu na waafrika hii ni moja ya kesi ambayo miaka hiyo ya 1994 ilikuwa gumzo sana.
Ilikuwa ni Kesi ya Karne iliyobeba Mvuto mkubwa sana ndani na Nje ya Marekani.Ilifuatiliwa kwa umakini mkubwa na watu mbalimbali duniani. Kesi ya O.J

O.J Simpson ni nani?

O.J Simpsoni aka The Juice alikuwa mchezaji maarufu sana wa american football. mbali na hilo pia alikuwa ni muigizaji na Mtangazaji wa michezo hasa mchezo wa mpira wa miguu wa kimarekani siyo huu tunaoujua wa Brazili,VPL au EPL. alisoma katika chuo kikuu cha southern California ambako ndiko alikoanzia kucheza mpira huo maarufu nchini marekani katika timu ya USC Trojans. pamoja na vituko vingi huyu jamaa alikuwa ni Tajiri na maarufu sana kipindi hicho na alitokea kuanguka kimapenzi na kumuoa dada mmoja Bint wa kizungu aliyekuwa mtoto mbichi kabisa kifua saa sita kipindi hicho akiwa na miaka 18 aliyefahamika kwa jina la Nicole Brown na wakafanikiwa kupata watoto wawili. O.J simpson alipenda sana kujiambatanisha na wazungu. marafiki wake wengi walikuwa ni wazungu wenye pesa au maarufu ingawa pia alikuwa na marafiki weusi. alikutana nao sehemu mbalimbali na hasa alipokuwa akienda kucheza golf n.k

Tukio la Mauaji ya Nicole na R.Goldman.

Tarehe 13 mwezi wa 6 mwaka 1994 Simpson alipigiwa simu kuwa aliyekuwa mkewe nicole brown amekutwa ameuawa nyumban kwake na pia akiwa na mwanaume mwingine ambaye inasemekena alikuwa ni mchepuko au tuseme hawala yake maana alikuwa ameshaachana na O.J. siku hiyo O.J anapigiwa simu alikuwa kwenye safari ya kikazi huko chicago. jamaa akaamua kurudi los angeles mara moja. ingawa hata alipopigiwa simu hakuuliza ameufaje...unajua mara nyingi ukisikia mtu amefariki moja ya maswali muhimu ni amekufaje. na mara aliporudi kwa ajili ya hizo taarifa alikamatwa na kwa muda mfupi akatiwa pinguna kuwekwa kizuizini kutokana na ushahidi ulionesha kuwa O.J anahusika na kifo hicho cha nicole brown na goldman. hivyo akachukuliwa kwa ajili ya kuhojiwa. robert shapiro huyu alikuwa ni jamaa yake O.J akapigiwa simu na kuombwa aje amtetee O.J

Jaribio la kutoroka.

baadaye akaachiwa kwa dhamana. tarehe 17 sikua mbayo alitakiwa akamatwe kwa ajili ya kesi ya mauaji O.J aliamua kutoroka akiwa kwenye gari lake jeupe aina ya Ford Bronco likiendeshwa na rafikiye mweusi A.C Cowlings. inasemekena O.J alikuwa akitaka kutoroka. alifukuzwa na polisi na baadaye akaamua kurudi nyumbani baada ya kushawishiwa sana kuwa arudi nyumban kwake Rockingham. wakati huo shapiro alikuwa nyumbani na jamaa wengine akiwepo Robert Kardashian (huyu baba wa akina Kim Kardashian) ambaye alikuwa rafiki mkubwa sana wa o.j

O.J alipofika nyumban alikamatwa na kupelekwa kizuizini kwa ajili ya kusubiria kesi yake kuendeshwa. maana ushahidi ulionesha kuwa yeye alikuwa mtuhumiwa namba moja. kuna damu ambayo ilikutwa kwenye mlango wa gari lake na pia ndani na pia inaonekana gari lake lilikuwa limetoka na kurudi mida flan ambayo inaonesha ndiyo mauaji yalitokea. pia kulikuwa na gloves ambazo ziliokotwa nyumbani kwake zikiwa na damu. damu ilipoangaliwa kwenye vipimo vya dna ilionesha kuwa ni ya nicole na Ronald Goldman huyu alikuwa ni mhudumu wa bar. inasemekana alikuwa anatoka na nicole ambaye alikuwa ni mtalaka wa o.j.

Kesi kuanza kuandaliwa

yakaanza kutengenezwa mazingira ya kusikiliza kesi ya o.j .ilikuwa kesi iliyojaa shauku kubwa sana na mazingira tata ndani na nje ya mahakama kwa sababu ilikuwa na impact kubwa sana kisiasa na kitamaduni kutokana na kuwa muuaji alikuwa mtu mweusi maarufu na aliyeuawa alikuwa mtu mweupe. hivyo ikawa inaonekana labda ni kwa sababu yeye ni mtu mweusi ndo maana anasingiziwa kesi hiyo. hakimu ilibidi kwa uangalifu sana aanze kukusanya baraza la wazee pia kwa kuzingatia rangi zao. isionekani wamejaa weupe tu kwenye hilo baraza. hakimu aliyepewa jukumu la kusimamia kesi alikuwa ni mmarekani mwenye asili ya Japan.


Kesi yaanza kusikilizwa

july 8 1994 kukawa na kusikilizwa taarifa za awali ili kujua kama kuna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani O.J Simpson. na Ikaamuliwa na Jaji Kathleen Kennedy Powell kuwa kuna ushahidi wa kutosha kabisa kumfungulia mashtaka O.J kwa kesi ya mauaji. O.J akaletwa kwa pilato (mahakamani kwa ajili ya ufunguzi wa kesi). kama kawaida akaulizwa anasemaje kuhusiana na mashtaka aliyofunguliwa. akasimama kwa kujiamini kabisa akasema kwa asilimia 100 hakuwa na kosa. basi, jaji Lance A. Ito akapewa jukumu la kuiendesha kesi hiyo.

mashahidi mbalimbali wakaanza kuletwa kuhusiana na kesi hiyo. na moja wapo alikua ni dereva wa Taxi ambayo ilienda kumchukua o.j siku hiyo akielekea safarini. dereva huyo anasema alifika muda wa mapema lakini ilibidi asubiri sana kwa sababu oj hakuwepo. na baadaye aliona mtu akitokea nyuma ya nyumba gizani kidogo akiingia ndani kabla ya oj sasa kuja akiwa tayari kwa ajili ya kuelekea uwanja wa ndege. anasema pia mara ya kwanza alipoenda kumwangalia o.j hakuliona gari lake ain ya ford bronco ila badaye alipoenda alilikuta likiwa limepark.

baada ya huyo shahidi wakaja wengine kadhaa na mwishowe akaletwa shahidi ambaye alikuwa ni mpelelezi mark fuhrman. mark fuhrman ndiye aliyekuwa amegundua gloves ambazo zinasemekana zilikuwa ni za o.j na zilikuwa na damu. lakini pia oj alionekana kuwa amejikata kidogo mkononi. na hakuweza kutoa maelezo ya kutosheleza alijiumiza vipi hapo mkononi. na pia damu iliyopimwa kwenye mlango wa gari lake ilionekana ni yake. hivyo ikahisiwa pengine alipoenda kufanya hayo mauaji alijiumiza.

O.J na jopo la Mawakili Wazuri na Marafiki zake.

o.j alikuwa na jopo la mawakili wazuri sana hapo usa.wakiongozwa na Johnnie Cochran pia walikuwepo Robert Shapiro,F. Lee Bailey na Robert Kardashian ( baba ya watoto wakali sana huko nchini marekani pia wenye ukwasi wa kutosha tu ukijumlisha na urembo wao). jopo la mahakama pamoja na mawakili wa o.j wakapanga safari ya kwenda kutembelea nyumban kwa o.j kuangalia mazingira ya upatikanaji wa ushahidi n.k jopo la mahakimu/wazee wa mahakama walikuwa 8 weusi,1 muhispania, wawili mchanganyiko. na katka hao 8 wanawake na 4 wanaume.

Kesi ilirudi tena mahakamni na ikaja kutokea mpelelezi M. Fuhrman amewekwa kwenye kizimba kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano na F.L Bailey. na katka mahojiano hayo bailey alimuuliza fuhrman kama amewah kutumia neno la kibaguzi(nigger) katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. mpelelezi alikataa kuwa hakuwah kutumia neno hilo na wala yeye si mbaguzi. mawakili wa o.j walianza kutengeneza kesi iwe kama ina conspiracy ili kuwatoa watu kwenye mstari. wakaamua kuingiza pia humo suala la ubaguzi wa rangi kuwa unaweza kuwa ni sababu. na katika kundi la mawakili wa o.j watatu walikuwa wazungu isipokuwa mmoja tu Johnnie.

mgogoro na mgomo mahakamani

kesi ikiendelea kukatokea hali ya sintofahamu wakati ambapo baadhi ya jurors(sifahama hawa kwa kiswahili wataitwaje) walipoanza kupunguzwa kwa vigezo mbalimbali. mawakili wa pande zote mbili walikuwa makini kuangalia katika hao jurors ni akina nani wanaonekana kuwa upande wa pili wa kesi.hivyo wakawa wanafanyiana fitna kwa kutumia vigezo mbalimbali ili hao jurors ambao walionekana kama ni threats kwa upande wao waondolewe.hivyo kukawa kunaletwa ushahidi kuwa juror flan anaonekana ana conflict of interest kwenye kesi hivyo aondolewe. na hii ikaleta changamoto maana jurors wengine wakaamua kufanya mgomo kwa kuvaa nguo nyeusi.

baadaye mambo yakarekebishwa na kesi ikaendelea. kwenye kesi kuna kipindi kulisikika kurushiana maneno makali kuhusiana na ubaguzi baada ya kuhojiwa kwa mpelelezi m.fuhrman na hapo wakili j.cochran ambaye alikuwa akimtetea oj alirushiana maneno makali na christopher darden ambaye naye alikuwa ni mmarekani mweusi lakini akisimama upande wa serikali. na huyu alichukuliwa makusudi na mwanamama marcia wasaidiane ili isonekane wanaotaka o.k afungwe ni wamarekani weupe. hivyo kwa upande wa serikali alikuwepo mwanamama Marcia Clark ambaye alikuwa ni mzungu na pia darden ambaye alikuwa ni mmarekani mwenye asili ya afrika.

baadaye mawakili wa o.j wakaamua kumchimba mpelelezi johnnie fuhrman na ikaonekana alishawah kufanyiwa mahojiano na mwandishi mmoja kipindi cha nyuma. mwandishi huyo alikuwa akitaka kuandika kitabu.

Ushahidi wa gloves zilizotumika kwenye uhalifu

wakili wa serikali bwana darden katika kuthibitisha kuwa muuaji alikuwa ni o.j simpson akamtaka akajaribu zile gloves. zile gloves zilionekana kutomtosha o.j ikaleta hal ya sintofaham mahakamani kuwa inakuaje tena uthibitisho ule kutoka upande wa serikali unaonesha kuwa gloves ambazo zilitumika siku ya tukio zilikuwa ndogo. hii ilileta mkanganyiko upande wa mawakili wa serikali. na ikaleta ile hali ya mwanzo kuwa inawezekana o.j alisingiziwa kwa sababu yeye ni mtu mweusi.

ukaletwa ushahidi wa dna. ambao pia mawakili wa o.j waliupinga kwa hoja kuwa inawezekana nao ulibambikizwa kama ambavyo ilitokea kwa gloves. na hapa walirudia pia ile sehemu ambayo moja ya ushahidi ulioletwa mahakamani ulikuwa ni viatu vya o.j simpson ambavyo soli yake ilionekana kuwa ilikanyaga damu sehemu ya tukio na hivyo kuacha alama. mawakili wa o.j wakamuuliza polisi aliyeleta ule ushahidi kuwa mbona siku ya kwanza ule ushahidi hakuwa umeandikishwa kwenye kitabu cha vithibitisho vya mauaji yale kutendwa na o.j. akasema kuwa siku ile ya kwanza alisahau vile viatu kwenye buti ya gari yake hivyo akaondoka navyo nyumbani. mawakili wa o.j wakamuuliza mara ya mwisho kwenda na vidhibit vya ushahidi nyumbani ilikuwa lini ukiacha siku ile ya viatu vya o.j. yule askari akasema hakumbuki. wakamwambia inawezekana alipoenda navyo nyumban vile viatu alienda kuvitengenezea ushahidi hivyo haviwezi kuchukulika kama ni sehemu ya ushahidi kwa sababi unaonekana kuwa wanataka kumsingizia o.j hivyo wamemtengenezea ushahidi wamfunge.

Ushahidi wa kuwepo viashiria vya ubaguzi wa rangi kwenye kesi.

mawakili wa o.j wakaenda kufuatilia yale mahojiano ya mpelelezi fuhrman na yule mwandishi wa kitabu. wakafanikiwa kupata. katika yale mahojiano mpelelezi alisikika akisema mbaya sana kuhusiana na wamarekani weusi. na alisema kabisa kuwa kuna kipindi huwa anawatafutia hata ushahidi wa uongo ili tu wafungwe maana anawachukia sana na kuwaona kuwa wao ni wahalifu tu kila wakati. aliendelea kuongea maneno ambayo mpaka pia yakamuingiza mke wa jaji ito marchia ambaye aliamua kujitoa kwnye ile kesi hasa bada ya kuona na yeye mke wake amesemwa vibaya na mpelelezi fuhrman hivyo kuendelea na ile kesi kungesababisha iwe na mgongano wa kimaslah. baadaye akashauriwa kuwa kile kipengele chake hakina uhusiano na kesi iliyopo mbele. maana kesi ilihusu mauaji yaliyofanywa na o.j na si suala la ubaguzi wa rangi uliosemwa na mpelelezi. august 15,1995 jaji Ito anabadili mawazo anakubali kuendelea na ile kesi. wanaamua kusikiliza zile tape zenye mahojiano ya Mpelelezi na mwandishi wa vitabu. baadaye wanaamua kuondoa kile kisehemu chenye kumsema mke wa ito wasikilize maneno mengine tu bila baraza kuwepo. baadaye jaji ito anaamuru kuwa ile tape isikilizwe wakiwepo na wazee wa baraza. baadaye anaitwa tena mpelelezi mark fuhrman ambaye safari hii anakataa kuzungumza jambo lolote kwa kukumbusha kuwa ni haki yake kikatiba katika ibara ya 5 ili asijitie matatani au hatiani. hivyo anagoma jambo kujibu jambo lolote.

mawakili wa o.j wakataka kujua kama simpson angeweza kusimama kujitetea mwenyewe. hvyo wakaammua kufanya majaribio ya kumhoji kama vile yupo kizimbani. wakaona asingeweza kujibu maswali vizuri. hivyo wakaiambia mahakama kuwa simpsoni hatojitetea mwenyewe. majaji wanakubali lakini mawakili wa serikali wanapinga. wakimtaka simpsoni ajitetee. lakini inashindikana hivyo simpson hasimamiswhi kizimbani kujitetea.na hii inakuwa pia ahueni kwake maana yule mama marcia alikuwa anamsubiria kwa hamu sana akijua jamaa angejichanganya sehemu flan ambako wangembana huko huko.

wakati kesi ikiendelea kunapotokea mabishano o.j anasimama na kupaza saut yake kuwa sikumuua,nsingeweza kumuua na kamwe nsingeweza kutenda kosa kama hili" aaambiwa akae.


Mpelelezi M.Fuhrman ni nduguye Adolf Hitler

mahakaman majibishano na hisia kali zinatawala na mawakili wawili cochran wa o.j na darden wanaingia tena kwenye mgogoro pale cochran anapomfananisha fuhrman na hitler mbele ya mahakama.
kesi ikaendelea ikifuatiliwa na mamilioni ya watu duniani mpaka siku ya mwisho waznapoenda kupiga kura wazee wa baraza. wengi hasa wa asili ya afrika wanasema kuwa O.J Simpson HANA HATIA. na wazungu wachache wanasema ana hatia. hivyo wengi wape. O.J Anatolewa gerezani na kurudi uraiani.

Athari za matokeo ya kesi kwa wahusika

jambo hili linawaumiza sana Mawakili wa serikali Mama Marcia na Bwana Darden ambao wanaamua kujiuzulu nafasi zao kwa kuwa wanaamini kuwa O.J aliua sema wameshindwa kwa sababu ya teknik tu za kisheria na si kwa kuwa O.J si mhalifu. inawaumiza sana wanaamua kujiuzulu nafasi zao.

R.Kardashian anajisikia kuwa na hatia kwa kumtetea O.J maana anaanza kuamini kuwa ni kweli O.J alimuua Nicole wanapoteza urafiki wao kwanzia hapo hawawasiliani tena. O.J anakuwa huru kila mtu anashika hamsini zake.

Kunguru Hafugiki na sikio la kufa halisikii dawa.

baadaye mwaka 1997 anakuja tena kukutwa na kosa la pale kesi hi inapofunguliwa upya na anatakiwa kulipa dollar 33,500,000 kwa familia za marehemu. kana kwamba haitoshi anafanya tena uhalifu.akaendelea na uhalifu mwingine mwingi na kujikuta mpaka sasa yupo ndani ispokuwa mwaka 2017 anaweza akasikilizwa kwenye kamati ya parole kuangaliwa anafaa kuachiwa au aendelee kukaa ndani. ni wazi kuwa jamaa ile dhambi ya damu ya wale watu iliendelea kumtafuta pamoja na kuwa alishinda ile kesi mara ya kwanza kwa kuingiza maswala ya ubaguzi n.k ila ni wazi kuwa jamaa ni mhalifu. hii ni kesi iliyovuma sana kwenye vyombo vya habari miaka hiyo ya 90. ikifahamika kama kesi ya O.J Simpsoni dhidi ya Wananchi.

tutaendelea kuwasiliana tena katika kesi na matukio mbalimbali. inawezekana kukawa na makosa madogo madogo ya kiuandishi basi katika hilo nitahitajitu niaptiwe ghofilo yaani msamaha na lisiwatoe kwenye kisa chenyewe

Home

TANZIA: Aliyekuwa Mbunge wa Mufindi na Waziri wa Elimu Awamu ya Tatu, Joseph Mungai afariki dunia

10:25

Joseph Mungai enzi za uhai wake

Habari za kushtusha toka chanzo cha kuaminika Hospitali ya Muhimbili kinathibitisha aliyewahi kuwa waziri wa Elimu ndugu Joseph Mungai na Mbunge wa Mufindi amefariki dunia.!

Geofrey Mungai mtoto wa Marehemu amesema marehemu alipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuanza kutapika mfululizo na kudhaniwa kwamba alikuwa amekula kitu kibaya.

Joseph James Mungai alizaliwa tarehe 24 Oktoba 1943

Like us on Facebook

About me

Ismail mbaazi
Email: mbaazishumaa6@gmail.com
#+25565-9230-273