ujasiriamali January 2016 - UJASIRIAMALI

ISLAMIC STATE WATHIBITISHA JIHAD JOHN ALIUAWA

23:38


JohnImage copyrighP
Image captionJihadi John alitumiwa sana katika video za propaganda za IS
Kundi la Islamic State limethibitisha kwamba mwanamgambo aliyetafutwa sana na mataifa ya Magharibi, aliyejulikana kama Jihadi John, alifariki.
Kundi hilo limetangaza kifo chake kwenye jarida lake la mtandaoni kwa jina Dabiq.
Mwanamgambo huyo aliuawa kwenye shambulio lililotekelezwa kwa kutumia ndege isiyokuwa na rubani Novemba mwaka jana.
Marekani, baada ya kutekeleza shambulio hilo katika ngome ya IS mjini Raqqa, ilisema ilikuwa na “uhakika kiasi” kwamba alikuwa ameuawa.
Mwingereza huyo, ambaye jina lake la kuzaliwa ni Mohammed Emwazi, alionekana kwenye video nyingi za IS akiwakata shingo mateka kutoka mataifa ya Magharibi wakiwemo Waingereza David Haines, aliyekuwa mfanyakazi wa shirika la kutoa misaada, na dereva wa teksi Alan Henning.
Kwenye tangazo la tanzia kwenye jarida hilo, Emwazi anaitwa Abu Muharib al-Muhajir, jina alilojulikana nalo katika kundi hilo.
Maelezo ya kifo chake yanathibitisha taarifa kutoka kwa Marekani kuhusu yaliyotokea siku hiyo.
Kundi hilo limesema Emwazi aliuawa tarehe 12 Novemba “gari alimokuwa akisafiria liliposhambuliwa na ndege isiyo na rubani katika mji wa Raqqa, ambapo gari lake liliharibiwa na akafariki papo hapo.”
Picha ya mwanamgambo huyo akiwa ametabasamu, na ambaye anaonekana akiwa hajajifunika uso huku akiwa ameangalia chini, imechapishwa kwenye jarida hilo.
Emwazi alizaliwa nchini Kuwait mwaka 1988 lakini akahamia Uingereza mwaka 1994 akiwa na umri wa miaka sita.

Watu wenye silaha wavamia chuo kikuu Pakistan

23:35


Watu wenye silaha wameshambulia chuo kikuu kimoja eneo la Charsadda kaskazini magharibi mwa Pakistan.
Washambuliaji walijaribu kuingia ndani ya chuo kikuu cha Bacha Khan kwa nguvu na makabiliano kati yao na maafisa wa usalama bado yanaendelea, ripoti zinasema.
Milipuko miwili mikubwa imesikika, afisa wa polisi ameambia shirika la habari la Reuters.
Ripoti zinasema watu wawili wamejeruhiwa. Maafisa wa usalama wamezingira chuo kikuu hicho.
Eneo la Charsadda liko umbali wa kilomita 50 (maili 30) kutoka jiji la Peshawar, ambako wapiganaji wa Taliban waliua zaidi ya wanafunzi 130 baada ya kushambulia shule moja.

Mwanamume mzee zaidi duniani afariki Japan

09:52


YasutaroImage copyrightGetty
Image captionYasutaro alizaliwa Machi 1903
Mwanamume mkongwe zaidi duniani amefariki nchini Japan akiwa na umri wa miaka 112.
Yasutaro Koide, kutoka jiji la Nagoya, alizaliwa tarehe 13 Machi 1903 na alifanya kazi kama fundi wa nguo wakati wa ujana wake.
Alitambuliwa na Guiness Book of World Records kama mwanamume mzee zaidi duniani Agosti mwaka jana.
Yasutaro alifariki kutokana na maradhi ya moyo na nimonia mapema Jumanne.
Alipoulizwa kuhusu siri ya maisha marefu alipokuwa hai, anadaiwa kuwashauri watu waache kujiumiza sana na kazi na pia waishi kwa furaha.
Kwa sasa mtu mkongwe zaidi duniani ni Mwamerika, Susannah Mushatt Jones, ambaye ana umri wa miaka 116.
Alichukua nafasi hiyo mwaka jana baada ya kifo cha Misao Okawa kutoka Japan aliyekuwa na umri wa miaka 117.
Mtu aliyeishi muda mrefu zaidi duniani kwa mujibu wa Guinness alikuwa Mfaransa Jeanne Calment, aliyeishi miaka 122 na siku 164. Alifariki Agosti 1997

KANISA LENYE UMBO LA KIATU (HIGH HEEL) LAJENGWA TAIWAN

05:53

Image captionKanisa la kiatu
Kanisa la urefu wa mita 16 lililojengwa kwa kutumia vigae vya glasi linalofanana na viatu vyenye visigino virefu vinavyopendwa sana na wanawake limejengwa huko Taiwan kwa lengo la kuwavutia wanawake zaidi.
Likiwa limejengwa kwa kutumia vigae vya glasi takriban 320,kanisa hilo la rangi ya buluu lina upana wa mita 10 na limegharimu takriban dola 686,000.
Picha iliopigwa juu ya kanisa hilo pia imeonyesha ukubwa wa kanisa hilo pamoja na uzuri wa eneo lililojengwa.
Jumba hilo la kuabudu linatarajiwa kufunguliwa tarehe 8 mwezi Februari tayari kwa mwaka mpya wa Uchina.
Image captionkanisa la kiatu Taiwan
Kiatu hicho kimetengezwa na maafisa wa baraza la miji kusini magharibi mwa pwani ,katika eneo moja la kitalii lenya umaarufu mkubwa huko Taiwan.
Lakini Pan Tsuei-ping,msimamizi wa ujenzi huo,ameiambia BBC kwamba kanisa hilo halitatumika kwa huduma za ibada za kila siku bali hafla za harusi.
''Katika mipango yetu,tunataka kulifanya eneo hili kuwa la kuvutia kimapenzi,kila msichana angepanda kutafakari atakapokuwa bibi harusi alisema'', Pan aliiambia BBC.

ONGEZEKO LA UJINGA NI CHANZO CHA TAIFA KUKOSA MAARIFA

05:50



  1. [​IMG]

    TANZANIA inakabiliwa na changamoto ya kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi bila kujengewa vyema stadi za kujua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK). Pichani hapo juu ni shule ya msingi Ndonga Wilayani Nyasa mkoani Ruvuma na hapa ni wanafunzi wa darasa la tatu wakisomea mazingira haya, hali hii inachangia utoro na kuongeza idadi ya wajinga nchini.

    Changamoto hiyo inasababisha kuwepo kwa ongezeko la wahitimu wa elimu ya msingi wanaohitimu ngazi hiyo ya elimu bila kuwa na stadi za KKK hali inayochangia kuwepo kwa ongezeko la idadi ya wajinga nchini na hivyo nchi kukosa maarifa na kusababisha ongezeko la umasikini miongoni mwa jamii yetu.

    Kwa mfano, mwaka 2012, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya, ilitajwa kuwa na wanafunzi zaidi ya 11,000 waliohitimu ngazi ya elimu ya msingi bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.

    Kwa upande wake, taarifa ya Idara ya Elimu ya Watu Wazima wilayani Tunduru, Mkoa wa Ruvuma, inasema asilimia 27 ya watu wazima wilayani humo, sawa na watu 32,333 ya watu wote wa wilaya hiyo wanaokadiriwa kufikia 118,083, walikuwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu mwaka 2011.

    Utafiti uliofanywa mwaka huo huo wa 2011 na taasisi moja binafsi nchini katika shule za sekondari Namatuhi na Ndongosi, zilizoko Kata ya Muhukuru, wilayani Songea, Ruvuma, ulionyesha kwamba karibu nusu ya wanafunzi wote wa shule hizo walikuwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.

    [​IMG]


    Wanafunzi kuendelea kusomea katika vibanda kama hivi Taifa litaendelea kuwa na idadi kubwa ya watu wajinga

    Katika tafiti mbalimbali za aina hiyo, imekuwa ikibainishwa kwamba idadi wanafunzi wanaojiunga na masomo ya kidato cha kwanza katika mikoa mbalimbali nchini, wastani wa wanaojiunga na ngazi hiyo ya elimu bila kuwa na stadi hiyo ya KKK ni kati ya wanafunzi 200 na 400.

    Takwimu hizi zimetokana na Taarifa za Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) zilizokusanywa katika mikoa Tanzania Bara katika miaka ya hivi karibuni. Tangu nchi hii ipate Uhuru mwaka 1961, historia inaonyesha kwamba yapo mambo mengi mazuri yaliyofanyika katika utekelezaji wa Sera na Mipango ya Elimu ya Watu Wazima (EWW)

Home

MAANA MBALIMBALI KATIKA MITANDAO YA SIMU E, 2G, 3G, H, H+ NA 4G

08:41

watu wengi hua mnasikia terminologies yani 2G, 3G Mara H, H+ au E etc, Je, maana yake ni nini kwenye network?

Kwa kifupi ni speed zinazotumika kusafirisha data kwenye internet ambapo zinatofautiana uwezo kutokana na teknolojia:

1. Neno G inasimama badala ya GPRS (General Packet Radio Service) na ndio first generation ya mobile phone technology.
Hua inamaanisha spidi ya internet yako ni ndogo sana (86kbps)

2. Neno E inasimama badala ya EDGE (Enhanced Data Rates for GSM evolution) hua inamaanisha speed ya internet yako ni ndogo ila ina afadhali kidogo kuliko G(236kbps)
EDGE SIGN


3. Neno 2G (Second Generation)
Ni generation ya pili ya mobile phone technology ambayo nayo inatumia GPRS system lakini speed yake ni kubwa kidogo than letter G, (154kbps) ila ni ndogo than letter E yaani ipo katikati ya G na E.

4. Neno 3G (Third Generation of mobile technology)
Inatumia UMTS & imebase kwenye GSM system, na ina speed kubwa kuliko hizo (speed yake 386kbps)

5. Neno H inasimama badala ya HSPA (High Speed Packet Access)
Ni muendelezo baada ya 3G ambayo ina speed kubwa (like 3.2 Mbps)

6. Neno H+ inasimama badala ya enhanced HSPA, Yaani hii ina speed kubwa zaidi ya H kama nilivyoielezeainauwezo wa kutransfer data up to 7.2 Mbps, ndio inayotumika kwenye simu nyingi nowadays.
7. Neno 4G (Fourth Generation of Mobile phone Technology) pia inajulikana kwa jina la LTE (Long Term Evolution).
Model hii ndio current kwa sasa ambayo inatumia H+so itakuwa na speed kubwa zaidi (like 14.4mbps to 21mbps)

8. Neno WCDMA inasimama badala ya Wide-band Code-division Multiple Access.
Inatumia teknolojia ya 3G ila imeongezewa GSM ambayo inaiongezea speed ya kusafirisha data na ndiomaana simu nyingi zimeitumia kabla ya kuja kwa 4G

1. Mobile signal strength

Very high signal icon
mtandao  upo juu sana
High signal icon
mtandao upo juu
Medium signal icon
mtandao  upo kati
Low signal icon
mtandao upo chini kidogo
Very low signal icon
mtandao upo chini kabisa
No signal detected icon
mtandano upo chini

No signal icon
hakuna mtandao simu imeshindwa kuunganishwa
Flight mode icon
Your phone is in Flight mode. Mobile, WiFi, FM radio and Bluetooth connections are all turned off simultaneously when you turn on Flight mode. (However, you can still turn WiFi, FM radio and Bluetooth on separately.
SIM card missing icon
line hakuna
SIM card locked icon
line imefugwa

2. Mobile data connection

GPRS icon
GPRS
EDGE icon
EDGE
3G icon
3G
4G icon
4G
HSDA/HSUPA icon
HSDPA/HSUPA
RTT icon
RTT
EVDO icon
EVDO
EVDV icon
EVDV

MSEMO WA LEO!!!

13:42


   Mtoto akikojoa kitandani agombezwe, baba asipokojoa kitandani afanyiwe check up

Like us on Facebook

About me

Ismail mbaazi
Email: mbaazishumaa6@gmail.com
#+25565-9230-273