Mbwa ‘shujaa wa Paris’
09:16Diesel aliuawa kwenye operesheni ya polisi mtaa wa Saint Denis Jumatan |
Katika vita, huwa kuna watu wanaoibuka mashujaa na kuenziwa na watu na taifa kwa jumla.
Huko Ufaransa, kuna mbwa mmoja wa polisi ambaye amepata umaarufu mkubwa sana na kusifiwa baada yake kufariki kwenye operesheni ya polisi.
Mbwa huyo wa jina Diesel anaweza kuelezwa kuwa ‘afisa wa polisi’ wa kwanza kufa vitani katika operesheni dhidi ya washukiwa walioshambulia Paris Ijumaa
mtandaoni, kulianzishwa kitambulisha mada, "Je Suis Chien," (Mimi ni Mbwa) ambacho kinafuata kitambulisha mada cha "Je Suis Charlie" ambacho watu walitumia kuonyesha uungaji mkono wao kwa jarida la Charlie Hebdo kufuatia shambulio jingine mapema mwaka huu.
Kuna hata ukurasa uliofunguliwa kwenye Twitter wenye jina lake na mada hiyo 'Je Suis Chien'
0 comments