POLISI WASHUTUMIWA AFRIKA KUSINI
22:48Polisi washutumiwa Afrika kusini
Polisi wamekuwa wakitoa utetezi wao kuwa walikuwa wanajihami
Tume ya uchunguzi nchini Afrika kusini imetaka ufanyike uchunguzi dhidi ya Polisi kuhusu mauaji ya wafanyakazi 34 wa mgodi yaliyofanyika mwaka 2012.
Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma amesema uchunguzi umebaini kuwa Polisi walikuwa na mpango usiofaa kumaliza mgomo katika mgodi mgodi wa Marikana na ilikuwa makosa kuutekeleza.
Wakati wote Polisi wamekuwa wakidai kuwa walikuwa wakijihami wakati wa mgomo wa wafanyakazi waliokuwa wakidai kuongezwa kwa mishahara.
Rais Zuma ameliita tukio hilo kuwa baya na kusema kuwa halina nafasi katika Demokrasia ya nchi hiyo.
Mauaji ya Marikana yanaelezwa kuwa mabaya kutokea nchini Afrika kusini tangu baada ya kumalizika kwa ubaguzi wa rangi miaka 20 iliyopita.
Wafanyakazi wa mgodi waligoma kwa siku kadhaa,na watu 10 tayari walipoteza maisha wakiwemo watu ambao hawakuwa kwenye mgomo, walinzi wa mgodi na Polisi, kabla ya tukio la tarehe 16 Agosti
0 comments